Kolo Toure: Gwiji wa Ligi Kuu ya England
Kolo Toure: Gwiji wa Ligi Kuu ya England
Mapema wiki hii mchezaji wa zamani wa Arsenal na Man City Kolo Toure amethibitishwa kwa nafasi ya kudumu katika benchi la ufundi la Meneja Pep Guardiola kwenye klabu ya Manchester City.
18 Julai 2025

Mwamba huyu wa Cote d’Ivoire alivuma zaidi alipokuwa mchezaji katika ligi kuu ya England na timu yake ya taifa.

Kolo Abib Toure mwenye umri wa miaka 44 ndiye mchezaji wa pili kucheza katika timu ya Tembo mara nyingi zaidi akiwa amekipiga mara 120 kuanzia mwaka 2000 hadi 2015.

Ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia mara tatu, Kombe la Mataifa ya Afrika mara saba na kusaidia timu hiyo kupata ushindi mwaka 2015. 

Alianza kucheza katika timu ya nchini kwao Cote d’Ivoire ASEC Mimosas, katika nafasi ya safu ya ulinzi na baadaye akajiunga na Arsenal mwaka 2002.

Pale Arsenal alikipiga katika mechi 326 na alikuwa pia katika kikosi cha ‘Invincibles’. Goli lake la kwanza kwa Arsenal lilikuwa Septemba 2002 katika uwanja wa Stamford Bridge wakati walipotoka sare ya 1-1 na Chelsea.

Mwaka 2009 Tembo huyo akaelekea Manchester City, mwaka mmoja baadaye mdogo wake Yaya, naye akaingia kwenye timu hiyo, na kuwasaidia City kushinda taji lao la kwanza la ligi kuu ya England katika kipindi cha miaka 44.

Mwaka 2013 Kolo akajiunga na mabingwa wa sasa wa EPL, Liverpool. Ni mmoja wa wachezaji 10 wa Ligi Kuu ya England kuwahi kushinda taji la EPL na klabu mbili tofauti akiwa na Arsenal na Manchester City.

Pia ameshinda taji la Ligi Kuu ya Uskochi na timu ya Celtic. Mpaka sasa ndiye mchezaji kutoka bara la Afrika aliyekipiga mara nyingi zaidi katika Ligi Kuu ya England, akiwa na jumla ya mechi 353.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us