UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki na Libya zatiliana saini mkataba wa madini, nishati na miundombinu
Uturuki ni nchi imara katika nyanja za kiuchumi na nishati, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Emaar Libya, anasema.
Uturuki na Libya zatiliana saini mkataba wa madini, nishati na miundombinu
Uturuki na Libya zimetiliana saini mikataba ya madini./Picha: AA
18 Julai 2025

Uturuki na Libya zimetiliana saini mkataba utakaoangazia ushirikiano katika maeneo ya madini, nishati na miundombinu.

Mkataba huo ulisainiwa kati ya Bodi ya Uhusiano wa Nje wa Kiuchumi ya Uturuki (DEIK), Baraza la Biashara la Uturuki na Libya, Shirika la Madini la Libya, Mamlaka ya Maonesho ya Libya na kampuni ya Emaar Libya, kwa lengo la kukuza kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Mkataba huo ulisainiwa na mwenyekiti wa DEIK, Murtaza Karanfil, Mwenyekiti wa Baraza la biashara la Uturuki na Libya, Fouad Al-Awwam, na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Emaar Libya.

Katika risala yake, Karanfil alisma kuwa Uturuki na Libya zimekuwa na historia ya uhusiano wa muda mrefu.

Kulingana na Karanfil, kampuni hiyo imewekeza katika maeneo mengi ya kibiashara, hususani katika eneo la mashariki na kusini mwa Libya.

"Kama wafanyabiashara wa Uturuki, licha ya kujihusisha na Libya yote, ushirikiano huu na kampuni ya Emaar utatupa faida kubwa."

Ukuzwaji wa kiwango cha biashara

Akizungumza na shirika la habari la Anadolu, Karanfil alisema kuwa bidhaa za Uturuki zinazosafirishwa nchini Libya ziliporomoka hadi kufikia dola bilioni 2.5 kutokana na hali ya machafuko kaskazini mwa Afrika baada ya mwaka 2014, na kubakia kwa kiwango hicho kwa miaka 10, na kuongeza kuwa kwa sasa, kiwango cha biashara kimefikia dola bilioni 4.

Alisema kuwa, makubaliano hayo yanalenga kukuza ushirikiano na eneo la mashariki mwa Libya, akiongeza kuwa “tunataka kuongeza zaidi kiwango hicho.”

 Akitolea mfano wa madini yaliyogunduliwa kusini mwa Libya katika miaka ya hivi karibuni, Karanfil alisema:

“Tumewaomba watupe ramani za migodi hususani ili iliyopo kusini, na watuambie ni maeneo gani wanataka tuyape kipaumbele katika uwekezaji na ushirikiano.”

"Kwa upande wetu, tunalenga kufanya mikutano ya kibiashara mashariki mwa Libya, kama kutakuwa na hilo hitaji.”

Kampuni zaidi kwenye sekta ya madini

Akisisitiza kuwa eneo la kusini mwa Libya lina hifadhi kubwa ya madini yenye kuvutia nchi nyingine, Karanfil alisema: “Leo hii, tuna kampuni sita tu za Kituruki zilizosajiliwa na Shirika la Madini la Libya.”

"Tunapambana kuongeza idadi hii nchni Libya, hususani katika nyanja ya nishati."

Kulingana na Al-Awwam, Uturuki ni nchi imara katika nyanja za kiuchumi na nishati.

"Tutatiliana saini mikataba hii na Uturuki kwa lengo la kufungua soko la Uturuki nchini Libya,” alisema.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us