AFRIKA
1 dk kusoma
Barcelona yaingia mkataba na DRC kukuza utalii
DRC imesaini mikataba mingine ya aina hiyo na vilabu vingine vya Ulaya, ikiwemo AS Monaco na AC Milan.
Barcelona yaingia mkataba na DRC kukuza utalii
Mkataba huo uliotiwa saini tarehe 29 Juni, unatarajiwa kudumu kwa misimu minne. / Reuters
18 Julai 2025

Klabu ya soka ya Barcelona imekubali mkataba wa udhamini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wenye thamani ya zaidi ya euro milioni 40 (sawa na dola milioni 46.37), kwa lengo la kusaidia kukuza utalii nchini humo.

Kwa mujibu wa nakala ya mkataba iliyoonwa na shirika la habari la Reuters siku ya Alhamisi, nembo ya utalii ya DRC itakayobeba kauli mbiu “Heart of Africa” (Moyo wa Afrika), itawekwa kwenye sehemu ya mgongo wa jezi za mazoezi za timu za wanaume na wanawake za Barcelona.

Mkataba huo uliotiwa saini tarehe 29 Juni, unatarajiwa kudumu kwa misimu minne, ambapo DRC itakuwa inalipa kati ya euro milioni 10 na 11.5 kila msimu.

Hata hivyo, taarifa rasmi kuhusu mkataba huo bado hazijatolewa hadharani na pande zote mbili. Aidha, DRC imesaini mikataba mingine ya aina hiyo na vilabu vingine vya Ulaya, ikiwemo AS Monaco na AC Milan.

Mwezi uliopita, vilabu hivyo vilitangaza ushirikiano wao na serikali ya Congo, lakini bila kuweka wazi kiasi halisi cha fedha kilichohusika.

Waziri wa Michezo wa DRC, Didier Budimbu, alisema kandarasi na AS Monaco ina thamani ya euro milioni 1.6 kwa kila msimu, lakini hakufichua maelezo ya kifedha kuhusu mikataba na Barcelona na AC Milan.

InayohusianaTRT Global - Kwa nini soka inachochea mzozo wa DRC na Rwanda?
CHANZO:Reuters
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us