UTURUKI
2 dk kusoma
Mapigano katika eneo la Sweida nchini Syria yanatishia usalama kanda nzima, Erdogan amwambia Putin
Katika mazungumzo kwa njia ya simu na kiongozi huyo wa Urusi, Rais wa Uturuki Erdogan anasema lengo la Uturuki ni kuhakikisha usalama, na nchi ya Syria kurudi kama zamani.
Mapigano katika eneo la Sweida nchini Syria yanatishia usalama kanda nzima, Erdogan amwambia Putin
Mapigano katika eneo la Sweida nchini Syria yanatishia usalama wa kanda nzima, Rais Erdogan amemwambia Putin wa Urusi. / TRT Balkan / AA
18 Julai 2025

Rsis wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemwambia mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin, kuma mapigano kufuatia kujiondoa kwa vikosi vya Syria kutoka Sweida yanatishia kanda nzima

Katika mazungumzo yao kwa njia ya simu siku ya Ijumaa, viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu uhusiano wa mataifa yao pamoja na ule wa kikanda na masuala ya ulimwenguni, kulingana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki katika mtandao wa X.

Erdogan anasema Uturuki ina nia ya kuhakikisha uthabiti na usalama pamoja na kuunga mkono juhudi za kujenga upya Syria, akisisitiza kuwa ni muhimu kwamba Israel isikiuke mipaka ya Syria.

Akisisitiza umuhimu wa kuanzisha hatua ya tatu ya mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine, Erdogan alisema Uturuki itaendelea kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani jijini Istanbul pindi tu pande zote zitakapokubaliana kuhusu tarehe.

Wakati huo huo, Putin alimshkuru Erdogan kwa utayari wake wa kuwa mpatanishi wa majadiliano ya Istanbul na kusisitiza dhamira ya Urusi ya kupata suluhu ya kisiasa na ya kidiplomasia, kulingana na taarifa kutoka Kremlin.

Pia aliangazia kuhusu uhusiano wa kiuchumi, akieleza kuridhishwa na matokeo ya tume ya kiserikali ya Urusi na Uturuki kuhusu ushirikiano wa Kibiashara na Kiuchumi ya Juni 27.

Putin na Erdogan walikubaliana kuendelea kuwasiliana kwa masuala yote waliyojadiliana kwenye mazungumzo ya simu.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us