Afrika
1 dk kusoma
Rwanda inahitaji madarasa mapya zaidi ya 26,000
Wizara ya elimu ya nchi hiyo inasema hii itaimarisha matokeo ya wanafunzi.
Rwanda inahitaji madarasa mapya zaidi ya 26,000
Rwanda inahitaji madarasa mengine zaidi ya 26,000
tokea masaa 8

Serikali ya Rwanda inasema inahitaji zaidi ya madarasa 26,500 mapya ili kupunguza msongamano wa wanafunzi .

Hili pia litatoa suluhu kwa mfumo wa sasa ambapo wanafunzi wengine wanasoma asubuhi na baadaye kuwapisha watakaoingia zamu ya mchana.

“ Mfumo wa wanafunzi kupishana hapo awali ulikuwa kwa kipindi chote cha elimu ya msingi, lakini kwa sasa, inafanyika kwa wale wa darasa la kwanza hadi la tatu kwa sababu kuna madarasa mengine yalijengwa," alisema.

Wizara ya elimu ya nchi hiyo inasema hii itaimarisha matokeo ya wanafunzi.

Ripoti iliyotolewa na Bodi ya Utawala bora ya nchini Rwanda inaangazia changamoto kama za msongamano wa wanafunzi shuleni na madarasa ya zamani, masuala ambayo wabunge wanataka maafisa wa elimu kuyashughulikia.

Waziri wa Elimu, Joseph Nsengimana alisema kuwa wizara ilifanya tathmini ya shule zake zote ili kufahamu hali halisi, huku akibainisha kuwa kuna madarasa 86,780 katika shule za umma na zinazosaidiwa na serikali nchi nzima.

Miongoni mwao, alisema, kulikuwa na madarasa 13,869 ambayo yanahitaji ukarabati.

Alisema kuna madarasa 5,830 ambayo lazima yabadilishwe kwa kuwa yameharibika.

“Kuna shule ambazo ni zamani na madarasa bado yanatumika. Hayawezi kuhimili kwa kipindi cha miaka mitatu zaidi. Kwa hiyo, tahmini yetu imebaini kuwa lazima yabomolewe na yanjengwe madarasa mapya,” alisema.

Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us