AFRIKA
1 dk kusoma
Salim Mvurya: Kenya iko tayari kuandaa michuano ya CHAN 2025
Michuano hiyo imepangwa kufanyika mwezi Agosti, 2025.
Salim Mvurya: Kenya iko tayari kuandaa michuano ya CHAN 2025
Waziri wa michezo nchini Kenya, Salim Mvurya./Picha:Wengine
26 Mei 2025

Waziri wa michezo nchini Kenya Salim Mvurya amesema kuwa nchi hiyo iko tayari kuandaa michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN 2025), tofauti na ilivyoripotiwa hapo awali.

Katika taarifa yake aliyoitoa Mei 26, 2025, Mvurya amesema kuwa hata wakaguzi wa CAF, walionesha kuridhishwa na maandalizi ya nchi hiyo, miezi michache kabla ya michuano hiyo kuanza kutimua vumbi.

Kulingana na Mvurya, serikali ya Kenya ipo tayari kutekeleza mapendekezo ya timu ya ukaguzi kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), ili Kenya iweze kuandaa michuano hiyo kikamilifu.

Michuano hiyo imepangwa kufanyika mwezi Agosti, 2025.

“Siku ya Ijumaa, tulifanya kikao na maofisa wa CAF, kama ilivyo utaratibu wa kawaida, kwani CAF hufanya ukaguzi wa mara kwa mara hadi ifikapo tarehe ya mwisho mwezi wa Julai. Katika mazungumzo yetu, tulikubaliana kuwa Kenya iko tayari kuandaa CHAN,”alisema Mvurya katika taarifa yake.

 

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us