AFRIKA
1 dk kusoma
Serikali ya Kenya kuuza zaidi hisa zake Safaricom, waziri wa fedha amesema
Serikali ya Kenya inapanga kuuza hisa zaidi katika kampuni kubwa ya mawasiliano nchini humo Safaricom, Waziri wa Fedha John Mbadi alinukuliwa na gazeti moja nchini humo siku ya Jumatatu.
Serikali ya Kenya kuuza zaidi hisa zake Safaricom, waziri wa fedha amesema
Serikali ya Kenya inapanga kuuza hisa zake katika kampuni ya Safaricom. /Reuters
26 Mei 2025

Serikali ya Kenya inalenga kupata dola bilioni 1.16 kwa ajili ya bajeti yake ya 2025/26 baada ya kuuza hisa zake za shirika kubwa la mawasiliano nchini humo, Safaricom, Waziri wa Fedha John Mbadi alisema katika mahojiano na gazeti la Business Daily.

Mbadi anasema kuwa fedha zitakazopatikana kwa kuuza hisa, zitasaidia kuchangia katika kubwa ya 2025/26. Waziri huyo wa fedha aliongeza kuwa muswada wa fedha wa 2025 ni mzuri wenye lengo la kuongeza kipato kwa raia.

Baadhi ya wabunge pia wamekuwa wakiishauri serikali kuuza hisa za shirika hilo pamoja na mashirika mengine ili kukabiliana na deni la taifa linalokuwa.

Kwa sasa, hisa za serikali ya Kenya katika kampuni ya Safaricom ni 35% baada ya kuuza 25% kwa umma mara ya kwanza 2008.

Kampuni ya Safaricom ya Kenya ina wateja milioni 44.7


CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us