Afrika
3 dk kusoma
Kwa nini Wakenya wanalazimishwa kuwa matapeli Myamnar?
Wakenya 64 wako katika kundi la raia wa kigeni 7000 walioachiliwa na makundi mawili yenye silaha nchini Myamnar
Kwa nini Wakenya wanalazimishwa kuwa matapeli Myamnar?
Wahasiriwa wa vituo vya ulaghai ambao walidanganywa au kusafirishwa kufanya kazi nchini Myanmar, walikwama kwenye eneo lililo ndani ya Hifadhi ya KK, kiwanda cha ulaghai, na kituo cha biashara ya binadamu kwenye mpaka wa Thailand-Myanmar baada ya msako mkali wa kimataifa dhidi ya magenge yanayoendeshwa na magenge ya wahalifu, yanayoendeshwa na Kikosi cha Walinzi wa Mipaka cha Karen (BGF) huko Myaddy26 Februari 2026
5 Machi 2025

Serikali ya Kenya inasema inafanya juhudi za kuwarejesha nyumbani raia wake waliokwama Myanmar.

“ Serikali inafanya mazungumzo na serikali ya Thailand ili kufungua mipaka yake na Myamnar kwa kuzingatia utu kuwaruhusu raia waliokwama Myamnar kuingia nchini Thailand na kurejeshwa nchini Kenya,” Wizara ya Mambo ya nje ya Kenya imesema katika taarifa.

Wakenya 64 wako katika kundi la raia wa kigeni 7000 walioachiliwa na makundi mawili yenye silaha nchini Myamnar.

Itabidi wavuke mpaka hadi Thailand kwa ajili ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.

Raia hao wanazuiliwa na vikundi vya waasi vinavyokabiliana na serikali ya Myamnar.

Hii ni kwa sababu mamlaka za Thailand hazijafungua tena mpaka huo tokea tarehe 12 Februari wakati kikundi cha kwanza cha raia wa kigeni 260 wakiwemo Wakenya 23 walikabidhiwa kwa jeshi la Thailand na Jeshi la Wabuddha la Democratic Karn.

Wakenya hao walifikaje Myanmar?

Shughuli za matapeli mitandaoni, ambazo zimeshika kasi katika maeneo yasiyodhibitiwa na Myanmar kwa miaka kadhaa, zinawavutia wafanyakazi wa kigeni kwa ahadi ya ajira zenye malipo makubwa.

Lakini wafanyakazi wanapowasili matapeli huwateka, na kuwalazimisha kufanya utapeli mtandaoni.

“ Nilikuja huku nikiahidiwa kuwa nitapata kazi ya ualimu, lakini kufika nikapata ilikuwa kazi ya utapeli ,” mmoja wa Wakenya hao aliyyehojiwa na vyombo vya habari vya Kenya alieleza, akiomba sura na jina yake lihifadhiwe.

“ Ukiwaambia unataka kwenda nyumbani wanakuitisha uwalipe dola 8,000 ilhali hauna,” ameongeza.

Balozi wa Kenya nchini Thailand Kiptiness Lindsay anasema kuna zaidi ya wakenya 100 katika mpaka wa Myamnar na Thailand.

“ Hapo awali tulikuwa na wakenya 64, lakini sasa tumepokea orodha ya majina ya watu 80 ambao wako katika kambi inayoendeshwa na mojawapo ya vikundi vyenye silaha,” Lindsay alieleza.

Kiptinesi amesema wengi wanaosafirishwa kutoka Kenya hadi Myanaar kupitia Thailand na wengi ni vijana katia ya 19 hadi 35 walio na masomo mazuri.

“ Wakifika katika vituo hivi wanakaribishwa na watu wenye silaha kwenye lango, wanapewa simu za rununu 5 na kompyuta moja. Halafu wanafanyiwa mafunzo ya ulaghai kwa siku 10 Baada ya hapo wanaambiwa waanze kutafuta wateja, ikiwa waathiriwa wengi ni wa kutoka nchi za kizungu,” balozi amesema.

Balozi Kiptenesi ameambia vyombo vya habari kuwa maeneo amabpo wapo hayapo chini ya usalama wa serikali ya Myamnar.

Hili ni eneo hatari, kuna zaidi ya makundi 30 zinazopigana na serikali ya Myamnar na mahali amabapo Wakenya hawa wapo pamethibitiwa na vikundi hivi vya waasi, “ balozi anaongezea.

Biashara ya utapeli

Februari 2025 Thailand ilipokea wafanyakazi 260 wa kutoak kwa vituo vya utapeli, zaidi ya nusu ya hao wanatoka Ethiopia, ambayo haina ubalozi nchini humo.

Mamlaka ya Thailand pia iliruhusu China kuwarejesha makwao raia wake 621 kupitia msururu wa safari za ndege kutoka mji wa mpakani wiki iliyopita.

Vituo vya utapeli vimekuwa vikifanya kazi katika eneo hilo kwa miaka mingi, lakini vinakabiliwa na uchunguzi upya baada ya kuokolewa kwa mwigizaji wa China, Wang Xing, ambaye alishawishiwa hadi Thailand kwa ahadi ya kazi, na kisha kutekwa nyara na kupelekwa katika kituo cha utapeli nchini Myanmar.

Nchi za Kusini-mashariki mwa Asia tangu wakati huo zimeongeza juhudi za kukabiliana na vituo vya ulaghai, ikiwa ni pamoja na Thailand kukata umeme, mafuta na usambazaji wa mtandao kwenye maeneo yanayohusishwa na vituo vya ulaghai.

Tangu Machi 2022, hasara ya kifedha iliyosababishwa na wahasiriwa wa ulaghai wa mawasiliano ya simu nchini Thailand pekee inafikia zadi ya dola bilioni 2.39, Kanali wa Polisi wa Thailand Kreangkrai Puttaisong alisema.

 

 

Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us