Afrika
1 dk kusoma
Tour du Rwanda: Hatua ya mwisho yasitishwa kwenye barabara zenye utelezi
Waandaaji waliomba mashindano hayo kuhitimishwa mapema huku ikiwa imebaki mzunguko mmoja kufuatia mvua kubwa iliyosababisha barabara kutokuwa salama.
Tour du Rwanda: Hatua ya mwisho yasitishwa kwenye barabara zenye utelezi
Mashindano ya uendeshaji Baiskeli ya Tour du Rwanda
3 Machi 2025

Hatua ya mwisho ya Tour du Rwanda mjini Kigali, eneo la mashindano ya dunia ya mbio za baiskeli mwaka huu, haikukamilishwa siku ya Jumapili baada ya mvua kufanya barabara kuwa na utelezi.

Uamuzi huo ulichukuliwa na maafisa kutoka bodi inayoongoza mashindano ya baiskeli, UCI, waandaaji walisema.

"Kutokana na hali ya hewa iliyosababisha barabara kuteleza, rais wa UCI aliamua kusimamisha hatua ya mwisho ya Tour of Rwanda huku ikiwa imebakia hatua moja," waandaaji walisema.

Mashindano ya Dunia ya barabarani yanatarajiwa kufanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza mjini Kigali kuanzia Septemba 21-28.

Kumalizwa mapema kwa mbio hizo kulimpa Fabien Doubey, Mfaransa mwenye umri wa miaka 31 ambaye anadhaminiwa na TotalEnergies ushindi wake wa kwanza katika kitengo cha waendesha baiskeli wa kulipwa.

Alimaliza sekunde sita mbele ya Mueritrea Henok Mulubrhan wa Eritrea.



Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us