AFRIKA
1 dk kusoma
11 wauawa katika shambulio la kujitoa mhanga Somalia
Takriban watu 11 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kujilipua nje ya kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumapili.
11 wauawa katika shambulio la kujitoa mhanga Somalia
Kundi la kigaidi la Al-Shabaab limekuwa sababu kuu ya ukosefu wa usalama nchini Somalia kwa miaka kadhaa sasa. / Picha: AA
18 Mei 2025


Takriban watu 11 waliuawa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kujilipua nje ya kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumapili, afisa mmoja alisema.

Mashambulizi hayo katika kambi ya jeshi la Somalia ya Damaanyo katika wilaya ya Hodan yalilenga wanajeshi waliokuwa wamejipanga nje ya jengo hilo.

Afisa wa usalama katika wilaya ya karibu ya Warta Nabada, ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliiambia Anadolu kwamba raia wawili na wanajeshi ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo la bomu. Alisema waliojeruhiwa walihamishiwa hospitalini.

Kundi la kigaidi lenye mafungamano na Al-Qaeda la al-Shabaab lilidai kuhusika na shambulio hilo.

Al-Shabaab imekuwa ikipigana na serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 16 na mara nyingi huwalenga maafisa wa serikali na wanajeshi.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us