Afrika
1 dk kusoma
Ofisi ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani kwa upande wa Afrika yafungwa
Uamuzi huo uliwasilishwa kwa njia ya barua pepe na Mkurugenzi Mtendaji wa WFP ulimwenguni Cindy McCain, siku ya Ijumaa.
Ofisi ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani kwa upande wa Afrika yafungwa
Uamuzi huo unakuja wakati ukanda wa Kusini mwa Afrika ukiwa unakabiliwa na hali mbaya ya ukame, hususani nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe na Namibia.
3 Machi 2025

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), ambalo hupata ufadhili mkubwa kutoka Marekani, linatarajia kufunga ofisi yake ya Afrika.

Uamuzi huo uliwasilishwa kwa njia ya barua pepe na Mkurugenzi Mtendaji wa WFP ulimwenguni Cindy McCain, siku ya Ijumaa.

"Tumefikia uamuzi mgumu wa kufunga ofisi yetu ya Afrika iliyoko Johannesburg," ilisomeka barua pepe hiyo kulingana na shirika la habari la Bloomberg.

Katika ujumbe wake mfupi kwa Shirika la Habari la Reuters, afisa mawasiliano wa WFP alithibitisha kufungwa kwa ofisi hiyo, japo hakuwa tayari kuhusisha uamuzi huo na mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kupunguza misaada.

Uamuzi huo unakuja wakati ukanda wa Kusini mwa Afrika ukiwa unakabiliwa na hali mbaya ya ukame, hususani nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe na Namibia.

Shirika la WFP limekuwa likitoa misaada ya chakula na kifedha kwa watu walioathirika na ukame, ikilenga kuwafikia zaidi ya watu milioni 7.2 ndani ya mwezi Machi.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us