AFRIKA
2 dk kusoma
Serikali ya Trump yawapeleka wahamiaji wa Asia Sudan Kusini, yakiuka agizo la mahakama
Wanasheria wa masuala ya wahamiaji wanasema wanaume wote wawili wamesafirishwa kutoka Marekani pamoja na watu wengine 10 katika 'mataifa mengine'
Serikali ya Trump yawapeleka wahamiaji wa Asia Sudan Kusini, yakiuka agizo la mahakama
21 Mei 2025

Wahamiaji wawili kutoka bara Asia ambao walikuwa wamezuiliwa katika kituo cha uhamiaji kwenye jimbo la Texas wamesafirishwa hadi nchini Sudan Kusini ikiwa ni ukiukwaji wa agizo la mahakama, mawakili wao walisema siku ya Jumanne.

Wanaume hao wawili ambao asili yao ni nchi ya Myanmar na Vietnam na walikuwa wanasubiri kusikilizwa kwa kesi yao hadi pale mawakili wao walipowaarifu kuhusu kupelekwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo lenyewe limekumbwa na mapigano.

Kufikia Jumanne asubuhi, mawakili wao walisema wanaume hao wawili walikuwa ndani ya ndege kuelekea Sudan Kusini wakiwa na wahamiaji wengine 10.

"Leo, nimeangalia kwenye mtandao wa idara ya uhamiaji na nikaona (mteja wangu) hakuwepo kwenye orodha ya waliokuwa kituoni," alisema wakili wa mmoja wa waliokuwa wamezuiliwa, Jacqueline Brown, katika kesi aliyowasilisha mahakamani.

"Nikatuma barua pepe kwa kituo cha Port Isabel kutaka uthibitisho kama N.M. yuko kwenye sehemu hiyo ...afisa wa kituo hicho cha Port Isabel akajibu kuwa ameondolewa 'asubuhi hii.' Nikatuma barua pepe na kuuliza amepelekwa nchi gani, na ofisa huyo akajibu ...'Sudan Kusini.'"

Kusafirishwa kwa wanaume hao wawili kutoka bara Asia kunakiuka agizo la mahakama lililotolewa na jaji wa Boston, Massachusetts ambalo lilizuia serikali ya rais Trump kuwapeleka raia wa kigeni kwa "mataifa mengine" badala ya nchi zao za asili bila kutoa ilani ya "msingi" na fursa ya kueleza wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuteswa katika ncji hizo.

Katika kesi hiyo, wahamiaji walikuwa wanapelekwa katika "nchi nyingine" ya Libya, ambayo kama Sudan Kusini, ina matatizo linapokuja suala la ukiukwaji wa haki za binadamu.

Wizara ya Mambo ya Ndani bado haijasema lolote kuhusu mawakili kulalamika juu ya wateja wao kuodolewa Marekani bila kufuata utaratibu.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us