Ofisi ya Taifa ya Mashataka nchini Rwanda (NPPA) imethibitisha kurejeshwa nyumbani kwa Ahmed Napoleon Mbonyunkiza kutoka Marekani.
Mbonyunkiza amerejeshwa Rwanda kutoka nchini Marekani ambako alitumikia kifungo cha miaka 15 baada ya kuhukumiwa kwa kosa la ubakaji na kuhusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi.
Mbonyunkiza mwenye umri wa miaka 57, alisafirishwa hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali (KIA) chini ya ulinzi mkali siku ya Machi 4, akitokea nchini Marekani ambako alitumikia kifungo cha miaka 15 baada ya kuhukumiwa kwa kosa la ubakaji na kuhusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi.
Kesi ya Mbonyunkiza iliendeshwa na Mahakama ya Gacaca ya nchini Rwanda, bila uwepo wake.
Katika taarifa yake, NPPA imezipongeza taasisi za kisheria za nchini Marekani kwa ushirikiano waliouonesha wakati wa kumrudisha Mbonyunkiza nchini Rwanda.
“NPPA inazipongeza taasisi za Marekani kwa ushirikiano wao,” taarifa hiyo ilisomeka.
Urudishwaji nyumbani wa Mbonyukiza ni sehemu ya jitihada za kimataifa za kuwapeleka kwenye mikono ya sheria washukiwa wa mauaji hayo.