Ujerumani inajipanga kusitisha misaada kwa Rwanda kutokana na madai ya kujihusisha na kikundi cha M23 katika eneo la Mashariki la DRC.
"Ujerumani itasitisha uhusiano wake na Rwanda," wizara ya maendeleo ya Rwanda imesema katika taarifa yake.
"Kimsingi, tutafute misaada mipya, pamoja na kupitia ile iliyopo kwa sasa."
Serikali ya Ujerumani ilisema kuwa inalaani vikali “uvamizi” wa wa DRC, hasa katika maeneo ya Goma na Bukavu, ikiuita “ukiukwaji wa utawala wa DRC”.
Tayari, Rwanda imeshafahamishwa na Ujerumani kuhusu mpango huo.
Wastani wa misaada ya Ujerumani kwa Rwanda una thamani ya wastani wa Dola za Kimarekani Milioni 53 kwa mwaka, katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, uzalishaji wa chanjo na mabadiliko ya tabia nchi.
Uamuzi wa Ujerumani unakuja siku chache baada ya Uingereza kusitisha kuipa Rwanda misaada huku Canafa nayo ikiiwekea vikwazo nchi hiyo kufuatia mgogoro.