Uturuki
2 dk kusoma
Uturuki ni umuhimu kwa amani ya Ukraine, urekebishwaji wa usalama wa Ulaya— Fidan
Kulingana na mwanadiplomasia huyo mkuu nchini Uturuki, mambo yanayoendelea kwa sasa yanatoa picha tofauti ndani ya Umoja wa Ulaya, hususani msimamo wa Marekani kuhusu vita nchini Ukraine.
Uturuki ni umuhimu kwa amani ya Ukraine, urekebishwaji wa usalama wa Ulaya— Fidan
Kulingana na Fidan, mambo yanayoendelea kwa sasa yanatoa picha tofauti ndani ya Umoja wa Ulaya, hususani msimamo wa Marekani kuhusu vita nchini Ukraine.
3 Machi 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan ameweka msisitizo nafasi ya Uturuki katika upatikanaji wa amani Ukraine pamoja na uimarishwaji wa usalama barani Ulaya.

 Akizungumza baada ya kikao cha ngazi ya juu kilichofanyika jijini London siku ya Jumapili, Fidan alielezea umuhimu wa kikao hicho ambacho kiliwaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi 17 ndani ya Umoja wa Ulaya na Canada.

“Hichi ni kikao muhimu sana, kikiwa kimehudhuriwa na nchi 17 kutoka Umoja wa Ulaya na Canada, isipokuwa Marekani,” alisema.

Kulingana na Fidan, mambo yanayoendelea kwa sasa yanatoa picha tofauti ndani ya Umoja wa Ulaya, hususani msimamo wa Marekani kuhusu vita nchini Ukraine.

“Kumekuwepo mitazamo tofauti ndani ya Umoja wa Ulaya kufuatia msimamo wa hivi wa karibuni wa Marekani. Yote haya yalijadiliwa wakati wa mkutano,” alibainisha.

Nafasi ya Uturuki kwenye usalama wa Ukraine na Ulaya

Fidan alisisitiza kuwa Uturuki ni mdau muhimu katika jitihada za upatikanaji wa amani katika maeneo yaliyokosa utulivu barani Ulaya.

“Mchango wa Uturuki ni wa umuhimu sana katika mpango wa amani wa Uturuki na urekebishwaji wa usalama wa Ulaya,” alisisitiza.

Mbali na majadiliano ya kusitisha mapigano, Uturuki imehusishwa pia na jitihada za kidiplomasia za kuleta utulivu wa muda mrefu.

Mijadala ya mara kwa mara ya kidiplomasia

Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Uturuki pia aligusia uwepo wa mikutano ijayo yenye kuihusu Ukraine.

“Tutakuwa na mikutano ya mara kwa mara, pengine kila baada ya wiki mbili au tatu,” Fidan alisema.

Mkutano huo wa London unakuja wakati muhimu wakati Ukraine inapambana na Urusi, ikitarajia kuungwa mkono kimataifa.

Uturuki imejizolea sifa kama msuluhishi wa migogoro na upatikanaji wa makubaliano.

Huku jumuiya ya kimataifa ikikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa utulivu huko Ukraine, ni jitihada za kidiplomasia za Uturuki pekee zitakazotoa mustakabali halisi wa hali ya amani duniani.

CHANZO:AA
Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us