Afrika
2 dk kusoma
Rwanda yaishutumu Ujerumani kwa vikwazo
Ujerumani imesitisha misaada ya fedha kwa Rwanda ikiilaumu kwa kuhusika na kundi la M23 linalofanya mashambulizi DRC.
Rwanda yaishutumu Ujerumani kwa vikwazo
Ujerumani imesitisha ahadi mpya ya fedha kwa Rwanda
5 Machi 2025

Ujerumani imeiwekea vikwazo Rwanda ikiihusisha na mashambulizi yanayotekelezwa na kundi la M23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

“ Ujerumani kuingiza siasa katika masuala ya maendeleo si sahihi na ni jambo ambalo halina tija, ” Wizara ya Mambo ya Nje imesema katika taarifa.

“ Ujerumani inaenda kinyume na madai yake ya kuunga mkono mchakato unaoongozwa na Waafrika wa kutatua mzozo wa mashariki mwa DRC kwa kuiruhusu DRC ionekane kama inapitia matatizo na ukiukwaji wa mambo ya msingi, jambo ambalo linaendeleza mzozo huo bila sababu,” Wizara hiyo imeongeza.

“ Tunalaani vikali vitendo vya Rwanda na M23 mashariki mwa Congo. Kukiuka usitishwaji wa vita na uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hakukubaliki. Ujerumani inasitisha ahadi za misaada ya kifedha kwa Rwanda na inatathmini tena ushirikiano baina ya nchi hizo mbili,” Ujerumani ilisema katika taarifa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda imesema kwa nchi kama Ujerumani ambayo inajivunia kuwa na ufahamu mzuri kuhusu matatizo ya ukabila, inaonesha kukosa ujasiri kwa kupuuza tishio linalosababishwa na wapiganaji wanaoungwa mkono na DRC wa mauaji ya kimbari ya FDLR kwa Rwanda, pamoja na jamii za Watutsi wa Congo Mashariki mwa DRC.

“ Nchi kama Ujerumani ambayo kihistoria inafahamu vizuri kuhusu ukosefu wa usalama unaoendela katika eneo hili inatakiwa kujua hakuna haja ya kuegemea upande mmoja,” Rwanda imesema.

Rwanda imeahidi kuendelea kulinda usalama wa taifa lake. Nchi hiyo pia imesisitiza msimamo wake kushiriki kikamilifu katika mchakato wa amani wa kikanda unaoendelea wa kutafuta suluhu kwa mzozo nchini DRC.


Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us