UTURUKI
7 dk kusoma
Namna Uturuki inavyoandaa kizazi kipya cha kuleta mabadiliko Afrika
Katika kuadhimisha siku ya Afrika, wanafunzi kutoka barani Afrika wanazungumzia hatua zilizobadilisha maisha yao wakati wakisoma katika taasisi mbalimbali za elimu nchini Uturuki.
Namna Uturuki inavyoandaa kizazi kipya cha kuleta mabadiliko Afrika
Mradi wa sauti za vijana wa Afrika / AFP
26 Mei 2025

Wengine wanakuja wakiwa na shauku ya kupata fursa ya kuwa sehemu ya mtandao wa dunia, wengine wanafika wakiwa na hamu ya kufahamu historia. 

Kinachojitokeza ni ari yao ya kutumia fursa hiyo siyo tu kwa kupata shahada bali kwenda kufanya mabadiliko nyumbani.

Uturuki, ambayo sasa inaonekana kama sehemu inayopendwa na wanafunzi wengi kutoka Afrika wanaofika kusoma elimu ya juu, inaendelea kuonesha dira kwa mustakabali kwa vijana wa bara hilo, ikiwapa fursa ili waweze kutimiza ndoto zao ambapo ni nchi chache wanaweza kuwa na fursa hiyo.

25 Mei huwa kunaadhimishwa siku ya Afrika kote ndani ya bara na nje ya bara, siyo tu kama ishara ya umoja, lakini wito wa kuwekeza kwa vijana wa Afrika. 

TRT Global imezungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka barani Afrika wanaosoma Uturuki kuangazia namna elimu inavyosaidia katika azma zao na hii inamaanisha nini kwa mustakabali wa bara lao, na pia kufahamu changamoto ambazo wanakabiliana nazo. 

Mwaka uliopita, Uturuki ilikuwa na wanafunzi wa kimataifa zaidi ya 336,000, huku 62,480 (karibu asilimia 18.6) wakiwa kutoka mataifa 53 ya Afrika, kulingana na data kutoka Baraza la Elimu ya Juu (YÖK).

Hii ikimaanisha kuwa kila mwanafunzi mmoja wa kimataifa kati ya watano nchini Uturuki anatoka barani Afrika. 

Kuna simulizi za wanafunzi vijana kutoka bara la Afrika, ambao wamevuka mipaka siyo tu kwa kwenda nchi nyingine, bali kutimiza ndoto zao. 

Wanafunzi wamejifunza Uturuki

Kabeer Moriki, mwanafunzi kutoka Nigeria aliye mwaka wake wa mwisho katika masomo ya Uchumi na Fedha Chuo Kikuu cha Okan jijini Istanbul, kwa kusoma Uturuki ni zaidi ya kupata faida ya masomo.

"Elimu ya kimataifa inafungua milango ya kupata mafunzo zaidi, mitazamo, na kuwepo na mitandao ambayo huwezi kupata ukiwa nyumbani. Inatoa fursa kwa vijana wa Afrika kupata mafunzo ya mifumo mbalimbali, kujifunza taratibu bora duniani, alafu namna gani mbinu hizo zinaweza kutumika kutatua changamoto za nyumbani,” anasema.

“Tukirudi nyumbani, haturudi tu na shahada. Tunarudi tukiwa na ujuzi, fikra, na ujasiri wa kufanya mabadiliko."

Moriki ana matumaini kuwa kizazi chake, ambacho anasema kina “ari, ubunifu, na uthubutu” unaohitajika kufanya mabadiliko barani Afrika. Ushauri wake: “Iwe unasoma nje ya nchi au nyumbani, lazima ukumbuke asili yako,na msaidiane, na daima muwe na hamu ya kupata mafanikio zaidi.” 

Maha Vahit, mwanafunzi wa shahada ya uzamivu kutoka Sudan katika Chuo Kikuu cha Istanbul, ana malengo hayo hayo ya kufanya mabadiliko, lakini kwake ni zaidi kuhusu historia ya fursa za misaada ya kupata elimu.

Wakati akisoma Historia katika Chuo Kikuu cha Khartoum, alianza kuwa na shauku ya kufahamu zaidi kuhusu mambo ya kale kutoka kwa mitazamo mbalimbali.

“Vyanzo ambavyo tulikuwa tunajifunza kuhusu historia ya Ottoman vilikuwa vimeandikwa Kiingereza. Kwa kuwa hiyo ilikuwa ikionesha upande mmoja tu, nikaona kuwa kuna umuhimu wa kuangalia chanzo kingine. Na ndipo nilipopata fursa ya msaada wa masomo Uturuki,” anasema.

Msaada huo wa masomo umemsaidia kujifunza Kituruki na kuanza masomo yake ya Historia. “Sasa, naweza kulinganisha elimu niliyopata kutoka kwa vyanzo vile vingine vya Kiingereza na kutoka kwa makumbusho ya dola ya Ottoman na vyanzo vya Uturuki. Hili linanipa uwezo wa kuandika kuhusu hali halisi kitaaluma.”

Vahit, ambaye ameshuhudia namna hali tete ya kisiasa ilivyotatiza wanafunzi wengi kukosa elimu nchini Sudan, anadhani kuwa na wanafunzi waliosoma kimataifa kunaweza kuchochea kuhakikisha uthabiti na uvumilivu wakati panapokuwa na mizozo ya kitaifa.

“Nina ndoto ya kuona Sudan bora,” anasema. “Na nataka niwe sehemu ya kusaidia hali hiyo.”

Elimu kama sera ya mambo ya kigeni

Katika muongo mmoja uliopita, elimu imeibuka kama nguzo ya Uturuki ya kidiplomasia na kusaidia kuimarisha bara la Afrika.

Misaada ya masomo inaratibiwa na ofisi ya Rais katika mpango wa YTB, mradi huo umesaidia sana wanafunzi kutoka Afrika. 

Mradi huo umepokea maombi 121,000 kutoka nchi 170 mwaka 2024, ikilinganishwa na maombi 42,000 mwaka 2012. 

Kila mwaka, wanafunzi wa kimataifa karibu 5,000 wanapewa fursa hiyo wakifadhiliwa kila kitu kuanzia ada, sehemu ya kulala, bima ya afya, na gharama za kuishi.

Kuhusu fursa hizo, Vahit anasisitiza kuhusu nafasi ambayo ufadhili wa masomo unasaidia kujenga uwezo wa muda mrefu: “Fursa za ufadhili wa masomo, ikiwa ni Uturuki au nchi zingine, inaweza kuwa njia nzuri ya misaada. Naamini kwa vijana wa Sudan. Wakienda nchi za nje kusoma, wanaweza kurudi wakiwa na mafanikio na kuchangia vyema kwa taifa lao.” 

Mtazamo wake unaashiria azma waliyonayo wanafunzi wengi kutoka bara la Afrika nchini Uturuki: kutumia fursa za elimu kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kudumu yatakayosaidia katika uimarishaji wa nchi.

Tangu 2012, Shirika la Uturuki la TİKA limetekeleza miradi zaidi ya 200 ya maendeleo nchini Tunisia, mingi ya hiyo ikiangazia katika mafunzo ya amali. 

Miongoni mwao ni kituo cha Jebeniana mjini Sfax, ambacho kilipata kifaa cha kupima na kupewa mafunzo ya kutengeneza injini za dizeli, hatua ilioimarisha mtaala wa taasisi hiyo.

Fursa ya ukuaji

Wakati Uturuki ikiwa inapendwa sana na wanafunzi kutoka bara la Afrika, kupata fursa ya elimu haimaanishi kuwa mtu anapata fursa ya kukubaliwa moja kwa moja nyumbani. 

Katika kundi la wanafunzi wa chuo kikuu cha umma, hali ya kijamii na kiuchumi ya nchi zao inawafanya waangaliwe kwa mtazamo wa kubezwa. 

Maswali kama “kuna uwanja wa ndege nchini Burundi?” au ‘‘Mna idara ya kusambaza dawa au idara ya uhusiano mwema?’’ kukiwa na haja ya kuwepo kwa ushirikiano wa kitamaduni miongoni mwa vyuo mbalimbali. 

Kwa wanafunzi wengi kutoka Afrika, changamoto hizi ni zaidi ya kauli tu — zinaonesha kutokuwepo kwa ushirikiano, uwakilishi, na mfumo wa kijamii.

“Sioni wanafunzi wote wa Kiafrika wakija pamoja katika jukwaa moja,” alisema Vahit. “Tunahitaji kuwepo na mfumo ambao utaturuhusu kusaidiana bila kuzingatia lugha, dini, au utaifa.”

Moriki pia alipitia hali hiyo ya kutopata msaada na kuamua kulishughulikia hilo mara moja.

“Moja ya changamoto ambayo nilipata ilikuwa ni kukosekana kwa mtandao wa watu kushirikiana kwa wanafunzi wa Kiafrika katika chuo changu kikuu,” alisema. 

“Kukabiliana na hilo, nilichukua hatua ya kuunda muungano wa Waafrika, kundi ambalo wanafunzi wataeleza kero zao, watoe mawazo yao, na kusaidiana wao kwa wao.”

Juhudi hizo zinaongozwa na wanafunzi, lakini zinaonesha umuhimu wa taasisi kuanzisha miradi ambayo itaandaa ushirikiano wa kitamaduni kwa wanafunzi wa Kiafrika. 

Muungano wa wanafunzi wa kudumu

Tangu 2002, Uturuki imeimarisha sana ushirikiano wake na mataifa ya Afrika na kuongeza uwakilishi wake wa kidiplomasia kutoka 12 hadi 44 kote barani. 

Huku ofisi za ubalozi zikiwakilisha kiwango cha juu cha ushirikiano kwa ngazi ya taifa, miungano ya wanafunzi waliosoma vyuo vikuu vya Uturuki inaashiria

Vyuo vikuu vinawakuwa na mabalozi thabiti wa bara hilo, kuunganisha utamaduni, viwanda, na taasisi. 

Wahitimu kadhaa wa Afrika waliosoma katika vyuo vikuu vya Uturuki wamepanda katika nyadhifa zao serikali na kuwa maafisa waandamizi na mabalozi katika nchi zao, jambo linaloonesha ushawishi wa muda mrefu wa mkakati wa elimu wa Uturuki. 

Kwa mfano Dkt. Hussein Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye alipata shahada yake ya udaktari kutoka Chuo Kikuuu cha Marmara jijini Istanbul.

Kuunga mkono juhudi hizi za wahitimu, Uturuki imeanzisha mitandao katika nchi zaidi ya 50 ikiwa ni kiunganishi kati ya Uturuki na wahitimu wa kimataifa, kusaidia katika upatikanaji ajira na kuimarisha ushirikiano wa mataifa.

Kwa muktadha huu, Siku ya Afrika inaadhimishwa kwa kusherehekewa na wito wa kuchukua hatua, pamoja na kutoa muelekeo wa mustakabali wa bara hili. 

Kama Vahit anavyosema: “Siku ya Afrika inatukumbusha kuwa popote pale tulipo, tunawajibika kwa bara letu. Ni siku ambayo inatufanya tufkirie namna gani tunaweza kuchangia, hasa katika suala la elimu na mafunzo. Kwangu mimi, kunamaanisha kusimama pamoja na bara Afrika ambalo ndoto yake ni amani, uthabiti, na maendeleo.”

CHANZO:TRT World and Agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us