1 Mei 2025
Katika kikao rasmi cha Kamati ya Ulinzi ya Seneti ya Marekani hivi majuzi, Michael Langley alimtuhumu Kapteni Traore kwa kutumia akiba ya dhahabu ya taifa lake kufadhili mitandao ya ulinzi binafsi, badala ya kuwekeza katika maendeleo ya taifa lake na pia kumtaja Traoré kama tishio kwa maslahi ya kikanda na kimataifa.
Lakini wakati Marekani ikiendelea kutoa wito wa kuwajibishwa kwa Traore, mashaka yanaibuka kuhusu uwezo wake wa kuhimiza maadili hayo nje ya mipaka yake, ilhali yenyewe inapambana na mgawanyiko wa ndani, ubaguzi wa rangi, na kuporomoka kwa imani ya raia katika taasisi zake.