Israel ilisema Jumapili inazuia kuingia kwa bidhaa na vifaa vyote Gaza.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel haikutoa maelezo zaidi kuhusu uamuzi huo lakini imeonya kuhusu "matokeo ya ziada" ikiwa Hamas, kundi la upinzani la Palestina, halitakubali kile ambacho Israel inasema ni pendekezo la Marekani la kurefusha muda wa usitishaji mapigano.
Haijabainika mara moja ikiwa usambazaji wa misaada umesitishwa kabisa.
Awamu ya kwanza ya usitishaji vita huko Gaza, ambayo ilijumuisha kuongezeka kwa usaidizi wa kibinadamu, ilimalizika Jumamosi.
Pande hizo mbili bado hazijafanya mazungumzo ya awamu ya pili, ambapo Hamas ilikuwa iwaachilie mateka kadhaa waliosalia ili kujitoa kwa Israel na kusitisha mapigano kwa kudumu.
Majadiliano yasiyokamilika
Israel iliidhinisha pendekezo la siku ya Jumapili la kurefusha kwa muda makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza kama hatua ya kuziba baada ya awamu ya kwanza ya usitishaji vita na Hamas kukamilika.
Awamu ya kwanza ya usitishaji vita kati ya Israel na Hamas ilikuwa inatamatika mwishoni mwa juma bila ya kuwa na uhakika wowote kuhusu awamu ya pili inayotarajiwa kuleta mwisho wa kudumu zaidi wa vita.
Wakati huo huo, Hamas imesisitiza kutekelezwa kwa awamu ya pili ya kusitisha mapigano.