Utajiri wa Afrika: Hifadhi ya Maasai Mara, fahari ya Kenya
Utajiri wa Afrika: Hifadhi ya Maasai Mara, fahari ya Kenya
Julai 2025, hifadhi hiyo imejumuishwa rasmi katika Kitabu cha Rekodi za Dunia, Uingereza, yaani World Book of Records Limited, kama tovuti ya "Uhamiaji Mkubwa Zaidi wa Kila Mwaka wa Wanyamapori Duniani."
17 Julai 2025


Ukitembelea Kenya na haujafika Hifadhi ya Taifa ya Maasai Mara kusini-magharibi mwa Kenya, basi itakuwa hujaona uzuri wa nchi hii ya Afrika Mashariki. 

Hifadhi ya Maasai Mara inatambuliwa kimataifa kama mojawapo ya Hifadhi Kuu za Wanyamapori barani Afrika. 

Neno 'Mara' linamaanisha 'madoa' katika lugha ya Kimaasai (Maa).

Baada ya kutembelea Maasai Mara, utaelewa jinsi eneo hili lilivyopata jina lake.Miti mifupi ya vichaka ambayo ina mandhari ya kupendeza huipa aina ya muonekano 'wenye madoadoa.'Mfumo wa ikolojia wa Maasai Mara ni mkubwa.

Ni sawa na karibu kilomita za mraba 1510. 

Eneo hilo limepakana na Serengeti Tanzania upande wa kusini na kaskazini, mashariki na magharibi mashamba ya Wamaasai. 

Ingawa kingo za mito mitatu ya eneo hilo zimezungukwa na vichaka na miti, sehemu kubwa ya hifadhi hiyo ina uwanda wa nyasi ulio wazi uliosheheni miti ya mshita katika sehemu tambarare. 

Kuna misimu miwili ya mvua hapa nayo ni, kati ya Aprili na Mei ambao ni msimu mrefu, na Novemba hadi Disemba ambao ni msimu mvua za muda mfupi. 

Hapa sasa uamuzi ni wako kama mtalii, ikiwa utapenda kwenda katika Hifadhi hii kwa njia ya gari au kupitia maputo ya hewa ili uangalie mandhari zuri kutokea juu angani.

Katika miti ya Mara kamaKama wewe ni mpenzi wa kuangalia ndege, basi katika miti ya Mara utaona zaidi ya aina 500 za wa kuwinda.

Kana kwamba hiyo haitoshi, Maasai Mara pia inajulikana kwa kuwa na mkusanyiko mkubwa zaidi wa wanyama pori duniani wanaokula mimea na wanaowinda.

Ni kawaida hapa kuwaona maelfu ya nyumbu na pundamilia wakiwa wakiwa safarini au wamepumzika.Zaidi ya asilimia 40 ya mamalia wakubwa wa Afrika wanaweza kupatikana hapa. 

Walakini, kuna mengi zaidi Maasai Mara kuliko tambarare zisizo na mwisho. Kando na Hifadhi kuu ya Kitaifa ya Maasai Mara, kuna dazeni za hifadhi za jamii, mashamba makubwa kadhaa za vikundi na vijiji vichache vya Wamaasai katika eneo hilo. 

Kila mwaka kuanzia Julai hadi Oktoba, Maasai Mara huwa mandhari ya maonyesho ya kuvutia zaidi ya wanyamapori duniani - Uhamiaji Mkuu wa nyumbu.

Muonekano wa wanyama wengi wanaovuka mito kwenye tambarare ni jambo la kushangaza na kivutio kikubwa la kimataifa.

Uhamaji huu wa kila mwaka kutoka Serengeti hadi Hifadhi ya Kitaifa ya Maasai Mara uliipatia hifadhi hiyo hadhi ya moja ya maajabu Saba ya Dunia kama 'uhamiaji pekee wa aina yake duniani. 

Julai 2025, hifadhi hiyo imejumuishwa rasmi katika Kitabu cha Rekodi za Dunia, Uingereza, yaani World Book of Records Limited, kama tovuti ya "Uhamiaji Mkubwa Zaidi wa Kila Mwaka wa Wanyamapori Duniani." 

Wakati wa msimu huu wa uhamiaji paka wakubwa wa Kiafrika hujitokeza zaidi kwani ni wakati mzuri wa mawindo kwa wanyama kama nyumbu wanaofanya uhamiaji. 

Faru, Simba, chui na duma na nyati huwa na nguvu zaidi wakati huu wa mwaka na wanaweza kuwa na watoto wadogo wenye afya nzuri na chakula kingi.

Muda mzuri kwa watalii kuwepo eneo hilo ni asubuhi na mapema.Na hakuna ziara ya Maasai Mara iliyokamilika bila kujionea tamaduni za Wamaasai ambao makaazi yao hi maeneo haya.

Utalii huu utakupa uelewa zaidi kuhusu tamaduni ya jamii zinazoishi katika Hifadhi hiyo.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us