AFRIKA
1 dk kusoma
Wanajeshi wa Kenya wauawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa
Wanajeshi hao walikuwa wakishika doria kando ya barabara kati ya Kiunga na Sankuri wakati gari lao lilipokanyaga kilipuzi kilichokuwa kimetegwa.
Wanajeshi wa Kenya wauawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa
Vitengo mbali mbali vya usalama vimeanzisha uchungzuzi. / Reuters
16 Julai 2025

Wanajeshi watatu wa Kenya waliuawa Jumanne na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati gari lao lilipolipuliwa na kilipuzi mashariki mwa kaunti ya Lamu karibu na mpaka na Somalia, jeshi lilisema Jumanne.

Wanajeshi hao walikuwa wakishika doria kando ya barabara kati ya Kiunga na Sankuri wakati gari lao lilipokanyaga kilipuzi kilichokuwa kimetegwa.

"Kwa kusikitisha, wanajeshi watatu mashujaa walikufa kwa majeraha," Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) lilisema.

Taarifa hiyo ilisema wanajeshi waliojeruhiwa walihamishwa hadi katika vituo maalumu vya kijeshi, na walikuwa wanapokea matibabu, bila kutoa maelezo zaidi.

Ripoti za vyombo vya habari vya ndani zilisema kulikuwa na wanajeshi saba waliojeruhiwa.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa uchunguzi umeaznishwa kufuatia tukio hilo.

CHANZO:AFP
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us