Watu wasiojulikana wamempiga risasi na kumuua mbunge wa eneo la Kapisul la nchini Kenya, Charles Ong’ondo Were katika tukio lililotokea Aprili 30, 2025 jijini Nairobi nchini Kenya.
Kulingana na mashuhuda, tukio hilo lilitokea katika eneo la mzunguko wa City Mortuary jijini Nairobi, majira ya saa 1.30 usiku.
Inadaiwa kuwa, watu wawili, waliokuwa wakitumia pikipiki, walimshambulia kwa risasi na kumuua mbunge huyo wakati akiwa ndani ya gari lake.
Dereva wa mbunge huyo hakupata madhara yoyote kwenye tukio hilo.
Huko nyuma, mbunge huyo aliwahi kusema kuwa anahofia maisha yake kutokana na matendo yaliyokuwa yanaelekezwa upande wake.
Kulingana na mashuhuda, polisi wa usalama barabarani walishuhudia tukio hilo, huku chanzo cha mauaji hayo kikiwa bado hakijulikani.