AFRIKA
2 dk kusoma
Rwanda yawatimua wanadiplomasia wa Ubelgiji
Serikali ya Rwanda imesema “uamuzi wa leo unaonesha dhamira ya Rwanda ya kulinda maslahi ya kitaifa na utu wa Wanyarwanda, pamoja na kuzingatia kanuni za msingi, amani, na kuheshimiana.”
Rwanda yawatimua wanadiplomasia wa Ubelgiji
Rwanda imewatimua wanadiplomasia wa Ubelgiji / picha: Ikulu Rwanda / Public domain
17 Machi 2025

Serikali ya Rwanda leo imefahamisha Serikali ya Ubelgiji kuhusu uamuzi wake wa kuvunja uhusiano wa kidiplomasia, kuanzia sasa hivi.

“ Wanadiplomasia wote wa Ubelgiji nchini Rwanda wanatakiwa kuondoka ndani ya saa 48. Kwa kuzingatia Mkataba wa Vienna, Rwanda itahakikisha ulinzi wa majengo, mali, na kumbukumbu za ujumbe wa kidiplomasia wa Ubelgiji mjini Kigali,” wizara ya mambo ya nje ya Rwanda imesema katika taarifa.

Tangazo hili linakuja siku moja baada ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kuikashifu Ubelgiji akidai kuwa imekuwa ikiidhoofisha Rwanda mara kwa mara, kabla na wakati wa mzozo unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

“Uamuzi wa Rwanda umechukuliwa baada ya kuzingatia kwa makini mambo kadhaa, yote yakihusishwa na hatua za kusikitisha za Ubelgiji kuendeleza udanganyifu wake wa ukoloni mamboleo.” wizara ya mamabo ya nje ya Rwanda imesema katika taarifa.

Serikali ya Rwanda imesema “uamuzi wa leo unaonesha dhamira ya Rwanda ya kulinda maslahi ya kitaifa na utu wa Wanyarwanda, pamoja na kuzingatia kanuni za msingi, amani, na kuheshimiana.”

“ Ubelgiji inatakiwa kuwajibika na vurugu za kihistoria, haswa katika kuchukua hatua dhidi ya Rwanda. Leo, Ubelgiji imechukua upande wa wazi katika mzozo wa kikanda na inaendelea kuchochea kwa utaratibu dhidi ya Rwanda katika vikao tofauti, kwa kutumia uwongo na ili kupata maoni ya uhasama yasiyo ya haki kwa Rwanda,” wizara ya mambo ya nje imesema.

Rais Kagame aliambia wananchi wake wasiogope taifa lolote kwani hakuna makubwa zaidi yatakayopata yakilinganishwa na mauaji ya halaiki ya 1994.

“Hakuna kitu ambacho kinaweza kutupata ambacho ni kibaya zaidi ya janga tulilonusurika. Ndiyo maana hatutakiwi kuogopa kusema, kupigana kwa ajili yetu wenyewe na dhidi ya wale wanaotaka kutuangamiza,” Rais Kagame alisema.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us