Ulimwengu
1 dk kusoma
Volodymyr Zelenskyy ‘akubali yaishe’ kwa Donald Trump
Kauli hiyo pia inakuja baada ya Marekani kusitisha misaada ya kijeshi kwa nchi ya Ukraine.
Volodymyr Zelenskyy ‘akubali yaishe’ kwa Donald Trump
Uamuzi wa kusitisha misaada kwa Ukraine ulipokewa kwa shangwe na Urusi, huku msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov akisema ni uamuzi ambao utaisukuma Kyiv kujongea meza ya mazungumzo ya amani ".
4 Machi 2025

Katika kauli yake ya kwanza tangu atofautiane na Rais Donald Trump wa Marekani wiki iliyopita, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, amesema yuko tayari kumaliza uhasama na Donald Trump, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi na kiongozi huyo ili amani ipatikane nchini Ukraine.

Kauli hiyo pia inakuja baada ya Marekani kusitisha misaada ya kijeshi kwa nchi ya Ukraine.

"Mimi na wenzangu tuko tayari kufanya kazi chini ya uongozi shupavu wa Rais Trump ili amani ya kudumu ipatikane," aliandika Zelenskyy kwenye ukurasa wake wa X.

"Mkutano wetu wa Washington haukwenda vizuri, ni wakati wa kuweka mambo sawa,” alisema kiongozi huyo wa Ukraine.

Uamuzi wa kusitisha misaada kwa Ukraine ulipokewa kwa shangwe na Urusi, huku msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov akisema ni uamuzi ambao utaisukuma Kyiv kujongea meza ya mazungumzo ya amani ".

"Ikiwa Marekani itaacha kutoa misaada ya kijeshi, huu utakuwa uamuzi bora kabisa katika mchakato wa upatikanaji wa amani," alisema Peskov.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us