UTURUKI
3 dk kusoma
Ukraine, Urusi yahitimisha mazungumzo ya Istanbul; Kiev inaitisha mkutano wa kilele wa viongozi
Mkuu wa ujumbe wa Ukraine anasema kwamba Kiev iko tayari kukubaliana na usitishaji mapigano mara moja, na anaonyesha matumaini ya "maendeleo zaidi" katika kubadilishana wafungwa.
Ukraine, Urusi yahitimisha mazungumzo ya Istanbul; Kiev inaitisha mkutano wa kilele wa viongozi
Hakan Fidan anasema kuwa lengo la Ankara lilikuwa ni kwa pande husika kuendeleza mazungumzo ya awali na kuzingatia hatua madhubuti. /Picha: / Reuters
23 Julai 2025

Duru ya tatu ya mazungumzo mapya ya amani kati ya Urusi na Ukraine imekamilika mjini Istanbul, iliyodumu kwa chini ya saa moja, huku pande zote mbili zikieleza uwazi wa tahadhari kwa mazungumzo zaidi - ingawa tofauti kuu bado zipo.

Kufuatia mkutano huo wa Jumatano, mkuu wa ujumbe wa Ukraine alisema Kiev iko tayari kukubaliana na usitishaji mapigano mara moja na akapendekeza kufanyika kwa mkutano wa kilele wa viongozi mwishoni mwa Agosti.

"Tunataka mchakato unaozingatia matokeo," Andriy Yermak alisema, akihimiza Urusi kuonyesha "mtazamo wa kujenga" kwenda mbele.

Ukraine pia ilionyesha matumaini ya "maendeleo zaidi" juu ya kubadilishana wafungwa wa vita, na kujenga juu ya makubaliano ya hivi karibuni ambayo ni pamoja na kurudishwa kwa miili 1,200 ya wanajeshi.

Mawasiliano yataendelea

Mkuu wa ujumbe wa wa Urusi Vladimir Medinsky alisema pande hizo mbili zimekubaliana kudumisha mawasiliano yanayoendelea na kwamba "makubaliano yote ya masuala ya kibinadamu yametimizwa."

Pia alithibitisha kuwa ubadilishanaji mkubwa wa pili wa miili umekamilika na akapendekeza kukabidhi miili 3,000 ya ziada kwa Ukraine.

Medinsky ameongeza kuwa Moscow imependekeza kuunda vikundi vitatu vya kufanya kazi mtandaoni ili kushughulikia masuala ya kisiasa, kijeshi na kibinadamu na kusema kuwa majadiliano yamejumuisha pia kuwarejesha makwao raia waliofungwa.

Alibainisha kuwa sio raia wote wa Urusi kutoka eneo la Kursk wamerudishwa na akapendekeza kuwabadilisha kwa askari wa Ukraine.

Alipoulizwa kuhusu wito wa Ukraine wa mkutano kati ya marais Volodymyr Zelenskyy na Vladimir Putin, Medinsky alisema mkutano huo unapaswa kutumika tu kwa kutia saini hati, na sio kufanya majadiliano.

Usitishaji mapigano wa muda mfupi

Zaidi ya hayo, Urusi ilipendekeza kwamba Ukraine ifikirie kutangaza usitishaji mapigano wa muda mfupi kama sehemu ya juhudi za kujenga imani.

Ingawa ni mfupi, mkutano wa Istanbul uliashiria hatua nyingine katika juhudi za Uturuki kusitisha vita, ambayo sasa ni vinaingia mwaka wake wa nne.

InayohusianaTRT Global - Urusi inatarajia kuanza tena mazungumzo ya amani na Ukraine wiki hii: Kremlin

Juhudi za kidiplomasia za Ankara

Fidan alisisitiza kuwa Uturuki imekuwa na jukumu kubwa la kidiplomasia tangu mwanzo wa mzozo, na kuongeza: "Uturuki imefanya juhudi kubwa chini ya uongozi wa Rais Erdogan tangu mwanzo wa mzozo huu."

Alisema lengo la Ankara ni pande husika kuendeleza mazungumzo ya awali na kuzingatia hatua madhubuti za kusonga mbele.

"Lengo letu ni kwamba pande zote zitakuwa na mashauriano yenye mwelekeo wa matokeo juu ya makubaliano hayo," alisema, akimaanisha nyaraka zilizobadilishwa katika duru za awali za mazungumzo ambayo yaliweka msingi wa mapendekezo ya kusitisha mapigano na makubaliano ya masula ya kibinadamu.

"Lengo kuu," aliongeza, "ni kujenga amani kupitia usitishaji mapigano."

Maoni hayo yanakuja wakati wajumbe wa Urusi na Ukraine wakianza majadiliano yanayotarajiwa kulenga kupanua mabadilishano ya wafungwa, na kujenga mazigira ya kufunguliwa kwa njia za kibinadamu, na kuweka msingi wa kukomesha vita.

Duru ya mwisho ya mazungumzo mwezi Juni ilisababisha makubaliano ya kihistoria juu ya kurejesha miili ya wanajeshi waliokufa na kuwapa kipaumbele wafungwa wa vita waliojeruhiwa vibaya.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us