Umoja wa Mataifa unasema migogoro inayoendelea nchini Ukraine, Sudan na Mashariki ya Kati imeathiri moja kwa moja usalama wa chakula wa ndani, kikanda na kimataifa kwa njia ambazo hazijawahi kushuhudiwa kwa kiwango na kasi, hasa katika mazingira ambayo tayari ni tete ambapo uthabiti ni mdogo na udhaifu umechangiwa.
Pia kuongezea athari za migogoro, kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya hali ya hewa, na kiuchumi kutokuwa na uhakika kumeongeza shinikizo kwenye mifumo ya chakula.
Katika mkutano kati ya 28 na 29 Julai unaofanyika nchini Ethiopia, Umoia wa Mataifa, UN na nchi za Afrika zinatathmini hali ya mabadiliko ya mifumo ya chakula.
Marais William Ruto wa Kenya, Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, na Azali Assoumani wa Comoros ni kati ya wale wanaohududria.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ndie mwenyeji wa mkutano huu.
“Mkutano unalenga jinsi gani nchi hufafanua na kufikia malengo yao ndani ya muktadha wa kipekee, kwa umakini maalum kwa mataifa yanayokabiliwa na udhaifu na uhamaji,” UN imesema.
Katibu Mkuu wa UN amezindua ripoti ya 2025 kuonyesha hali ya mifumo ya chakula duniani.
Ripoti inabainisha kuwa kufikia mwaka wa 2025, nchi 128 zilikuwa zimetengeneza njia za mabadiliko ya mifumo ya chakula, huku 155 zikiwa zimeteua wajumbe maalumu wa chakula.
Kati ya hizi, nchi 39 zilirekebisha na kusasisha njia zao kuwa mipango zaidi ya utekelezaji. Katika ongezeko kubwa la uwajibikaji, nchi 112 ziliwasilisha ripoti za maendeleo kwa hiari mwaka wa 2025, ongezeko kutoka 101 mwaka 2023.
“Njaa inaongezeka, majanga ya kibiashara yanapandisha bei ya vyakula, theluthi moja ya watu wanakosa kupata lishe bora, na thuluthi moja ya chakula inapotea, huku mifumo dhaifu ya chakula ikigharimu dola trilioni 10 kila mwaka, zaidi ya mara tatu ya Pato la Taifa la Afrika,” Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres ameuambia mkutano huo kupitia ujumbe wa video.
“Mgogoro huu hautokani na uhaba bali na ukosefu wa usawa, changamoto za hali ya hewa, na ukosefu wa haki. Migogoro na mabadiliko ya hali ya hewa huzidisha njaa, lakini kila dola inayowekezwa katika lishe inaweza kutoa manufaa ya hadi dola 23, hivyo kufanya mifumo ya chakula kuwa muhimu kwa malengo ya maendeleo,” Guterres ameongezea.
Mkutano wa Addis Ababa utaangazia umuhimu wa utawala shirikishi ambao unayapa kipaumbele makundi yaliyotengwa kama vile wanawake, vijana, watu wa kiasili na watu wadogo, wakulima, kutoa mafunzo muhimu ya kuongoza juhudi za baadae za uzaishaji.
Mkutano huo pia utalinganisha mifumo ya chakula mikakati na sera za maendeleo endelevu, kuimarisha mbinu zinazozingatia haki ili kuhakikisha hakuna aliyeachwa nyuma kwa uzalishaji wa chakula.
Majadiliano haya yalianza vipi?
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mifumo ya Chakula wa 2021 (UNFSS), ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, uliashiria wakati muhimu katika kufikiria upya mifumo ya chakula kama nguvu inayoongoza kwa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Katibu Mkuu ameamua kuwa UN itakuwa inafanya tathmini kila baada ya miaka miwili.
Ya kwanza kati ya hizi ilikuwa mkutano wa 2023 ambao ulithibitisha kuwa mifumo ya chakula inasalia kuwa kipaumbele cha juu cha ulimwengu na iliishia kwa Wito wa Kuchukua hatua kwa ajili ya Kuharakisha Mabadiliko ya Mifumo ya Chakula.
Pia ilichochea hatua za kimataifa kuelekea uthabiti zaidi, jumuishi, mifumo ya chakula yenye usawa endelevu, na kuzishawishi nchi kuanzisha kuleta mabadiliko kitaifa.
Licha ya kasi hii, muktadha wa kimataifa umezidi kuwa tete.
Mabadiliko ya hali ya hewa, mivutano ya kijiografia na ukosefu wa uthabiti, misukosuko ya kiuchumi na miktadha tete inavuruga kimataifa masoko na minyororo ya ugavi, kutishia maisha na lishe, na kuongezeka kwa ukosefu wa usawa.