23 Julai 2025
Zaidi ya nyumbu milioni 1.5 wameanza safari yao kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania, wakielekea Maasai Mara nchini Kenya. Tukio hilo kubwa, huvutia mamilioni ya watalii kutoka pembe zote za dunia.
Inakadiriwa kuwa nyumbu wapatao milioni 1.5 na wanyama wengine kutoka Tanzania, kwenda katika Hifadhi ya Maasai Mara ya Kenya kwenda kutafuta chakula, maji na mazingira ya kuzaliana katika tukio lenye kujulikana zaidi kama ‘The Great Migration.’