MICHEZO
2 dk kusoma
CHAN: Rais WIlliam Ruto aahidi wachezaji wa timu ya taifa jumla ya hadi shilingi milioni 600
Rais wa Kenya William Ruto amewaahidi wachezaji wa timu ya taifa Harambee Stars mamilioni ya pesa kila mmoja kwa kila mechi watakayoshinda.
CHAN: Rais WIlliam Ruto aahidi wachezaji wa timu ya taifa jumla ya hadi shilingi milioni 600
Kila mchezaji wa Kenya atapokea milioni moja kwa kila mechi watakayoshinda CHAN / TRT Afrika Swahili
2 Agosti 2025

Rais wa Kenya William Ruto ametoa ahadi ya mamilioni ya pesa kwa kila mchezaji kwa kila mechi watakayoshinda au kutoka sare kama kuwatia motisha katika mashindano ya mataifa ya Afrika ya kikanda CHAN.

‘‘Nataka tukubaliane, kwa kila mechi mtakayoshinda, kila mchezaji hapa atapata shilingi milioni moja. Kwa kila mechi mtakayotoka sare, mtapata nusu milioni. Mkishinda fainali pesa yenu yote itakuwa shilingi milioni 600,’’ alisema Rais Ruto katika mkutano na wachezaji hao katika hoteli jijini Nairobi.

Hii ni mara ya kwa kwa Kenya kushiriki michuano hii ambapo wanakwenda kukutana na wababe, Chui wa DRC, ambao wameshiriki shindani hili mara zote tangu lizinduliwe, ikiwa hii ni mara ya nane, na wameshinda mara mbili - 2009 na 2016.

‘‘Nimesema kila kitu mara tatu, ndio sasa kila mtu acheze kama yeye,’’ aliongeza Rais Ruto.

Mcheza kwao hutunzwa

Lakini hii ahadi haikutolewa Kenya pekee.

Nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu amewaahidi wachezaji wa Taifa Stars kitita cha hadi Bilioni moja iwapo watashinda kombe hilo.

‘‘Kwa vijana wetu wa Taifa Stars wanaokwenda kutuwakilisha, niwaambie kuwa tuna imani kubwa na wao,’’ alisema Rais Samia. ‘‘Mcheza kwao hutunzwa hivyo basi kombe likibaki hapa kuna tunzo yenu kutoka kwa mama yenu,’’ aliendelea kusema Rais Samia.

Tanzania watacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Burkina Faso Jumamosi pili, katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo timu zote mbili zimewahi kushiriki michuani hii mara tatu, huki Stallions hao wakiwa ndio wamefika angalau awamu ya makundi.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us