Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza, Marcus Rashford, amejiunga na klabu ya Barcelona kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Manchester United, kwa mkataba unaojumuisha chaguo la kununuliwa mwishoni mwa msimu, klabu hiyo ya LaLiga ilitangaza Jumatano.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, Barcelona itachukua jukumu la kulipa mshahara wake wote kwa msimu huu, baada ya Rashford kukubali kupunguziwa mshahara wake. Kipengele cha ununuzi katika mkataba huo kinakadiriwa kuwa na thamani ya takriban euro milioni 30, sawa na dola milioni 35.25 za Marekani.
Rashford ameifungia timu ya taifa ya England mabao 17 katika mechi 62. Alisema anahisi yuko fiti na katika hali bora zaidi baada ya kipindi chake Aston Villa, ambako alifunga mabao mawili katika mechi 10 za Ligi Kuu ya England.