AFRIKA
2 dk kusoma
Tanzania yatangaza kumalizika kwa ugonjwa wa Marburg
Hata hivyo, wakati nchi hiyo ikitangaza kumalizika kwa ugonjwa wa Marburg, Tanzania bado inakabiliwa na ugonjwa wa Mpox.
Tanzania yatangaza kumalizika kwa ugonjwa wa Marburg
Hata hivyo, Mhagama amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kuwa makini, hata baada ya kutangazwa kumalizika kwa mlipuko wa Marburg./Picha: @WHOAFRO / Others
13 Machi 2025

Wizara ya Afya nchini Tanzania imetangaza mwisho wa mlipuko wa ugonjwa wa Virusi vya Marburg (MVD) katika mkoa wa Kagera, ambao pia uliua watu wawili katika eneo hilo.

Katika taarifa yake iliyowekwa kwenye ukurasa wa X wa Wizara hiyo Machi 13, 2025, Waziri wa Afya wa nchi hiyo Jenista Mhagama, amesema kuwa serikali ya nchi hiyo ilichikua hatua madhubuti za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo katika halmashauri ya Biharamulo, ambali ni eneo liiloathirika zaidi.

“Kufikia Machi 11, 2025 ambazo ni siku arobaini na mbili tangu kuwepo kwa mgonjwa wa mwisho…kitaalamu na kulingana na kanuni na taratibu za Shirika la Afya Duniani (WHO), tumekidhi vigezo vya kutangaza rasmi kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa huo,” alisema Mhagama kupitia ukurasa wa X wa Wizara ya Afya.

Hata hivyo, Mhagama amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kuwa makini, hata baada ya kutangazwa kumalizika kwa mlipuko wa Marburg.

Mlipuko wa Mpox

Hata hivyo, wakati nchi hiyo ikitangaza kumalizika kwa ugonjwa wa Marburg, Tanzania bado inakabiliwa na ugonjwa wa Mpox.

Siku chache zilizopita, serikali ya nchi hiyo iliripoti uwepo wa watu wawili waliopatikana na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Mpox.

Kulingana na Waziri Mhagama, wahisiwa hao walitengwa kwa ajili ya matibabu baada ya kubainika kuwa na ugonjwa huo.

Chanzo cha ugonjwa Mpox ni wanyama jamii ya nyani, ambapo binadamu anaweza kupata kutokana na shughuli zinazoweza kusababisha kugusana na wanyama, majimaji au nyama za wanyama wenye maambukizi.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us