Waziri wa Kilimo na Misitu wa Uturuki Yumakli ametangaza kuwa watu 10, ikiwa ni pamoja na wachunkaji watano wa misitu na wahudumu watano wa utafutaji na uokoaji, walikufa shahidi wakati wa kukabiliana na moto wa msitu katika jimbo la kati la Eskisehir.
"Rambirambi zangu kwa nchi yetu nzima. Tunapitia jioni yenye uchungu sana. Wafanyikazi wetu kumi wa kuchunga msitu walikufa shahidi walipokuwa wakijaribu kuzima moto. Kwa sasa tunalifunga eneo hilo."
"Hatuwezi kuamini jinsi hili lilivotokea katika msitu mdogo, sio mkubwa sana. Tayari walikuwa wamekimbia hatari jana, na tulifurahi sana, lakini leo tumepoteza mashahidi," waziri alisema.
"Wakati wa kukabiliana na moto wa msitu uliotokea Eskisehir na kufikia mpaka wa Afyonkarahisar, wafanyakazi wetu 19 wa misitu na watano wa kujitolea wa kutafuta na kuokoa walinaswa kwenye moto kutokana na upepo mkali. Sasa hivi wafanyakazi wetu wa msitu 14 wanapokea matibabu katika hospitali," alisema.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kupitia mtandao wa X kwamba "Nilihuzunishwa sana kujua kuhusu kuuawa kwa wachungaji watano wa misitu na wafanyakazi wa kujitolea watano wa AKUT wakati wakijaribu kuuzima moto wa msitu huko Eskisehir.
Natoa pole kwa familia zao na taifa letu, na Mwenyezi Mungu awarehemu kaka na dada zetu waliojitolea maisha yao kulinda misitu yetu."