Attieke, chakula cha mihogo Cote d'Ivoire
Attieke, chakula cha mihogo Cote d'Ivoire
Mwaka 2024, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni, UNESCO, liliitambua na kuiorodhesha attieke kama urithi wa kitamaduni kutokana na heshima yake na ustadi unaotumika katika kuiandaa.
24 Julai 2025

Nchini Cote d'Ivoire upishi wa mihogo hufanywa kwa ustadi na njia ya kipekee. Chakula cha mihogo kinajulikana kwa jina la Attieke.

Imekuwa ishara kubwa ya utamaduni wao ukirithishwa kutoka kizazi kimoja hadi chengine.Côte d'Ivoire inazalisha takriban tani milioni 2.5 za mihogo kwa mwaka kiasi ambacho asilimia kubwa inatumika ndani ya nchi.

Mwaka 2024, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni, UNESCO, liliitambua na kuiorodhesha attieke kama urithi wa kitamaduni kutokana na heshima yake na ustadi unaotumika katika kuiandaa.

Nini kinachoifanya Attieke kuwa ya kipekee?

Kwanza, muhogo unachemshwa kidogo au kuokwa, hulowekwa kwa siku moja hadi tatu na kuufanya kuwa chachu.Kisha, mihogo safi zaidi hupunjwa, kukatwa na kuoshwa.

Pamoja na mihogo iliyochachushwa, mafuta ya mawese yenye joto kupita kiasi, na maji, huchanganywa na kupondwa pondwa.

Baadaye, rojo huwekwa katika mifuko ya plastiki na kuachwa kwa muda wa saa 12 hadi 15 ili kuchachuka zaidi.Kisha, unga uliochachushwa hukamuliwa vizuri ili
maji yatoke.

Unga wa kukausha huchujwa, wanawake hutumia mikono yao kunyunyiza unga ili chembechembe ziwe bora zaidi.

Baada ya hayo, unga uliokaushwa huwekwa kwenye jua ili kukauka zaidi.Ifuatayo ni chembechembe kuchomwa kwa mvuke (steaming)- badala ya kupikwa - katika vyungu vilivyoundwa kushikilia maji ya moto chini ya attieke kavu. Mchakato huu unachukua hadi dakika 40.

Na hapa Attieke iliyo laini kwa kawaida huwekwa kwenye mifuko midogo ya plastiki kwa ajili ya kuuzwa sokoni au kutumika nyumbani.

Kwa kawaida, upishi wa Attieke ni jukumu la wanawake ambao hupitisha ujuzi kwa wasichana wadogo.Wanapokutana kuutengeneza ni fursa ya kujenga uhusiano bora wa kijamii na pia ni chanzo cha fedha kwao wakiuza.

Wanawake huandaa, hupika, uhifadhi, na kuuza attieke, huku wanaume jukumu lao ni kupanda, kuvuna, kusafirisha na kusagabmihogo.

Utayarishaji wa chakula hilki ulikuwa hasa kwa eneo ka Kusini mwa Cote devoire lakini hivi sasa umesambaa nchini kote sasa.

Umaarufu wa Attieke umefikia nchi jirani kama
Burkina Faso, Ghana na hata inauzwa kwa watu Ulaya na Marekani Kaskazini.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us