22 Julai 2025
Ajali hiyo iliyohusisha lori la kubeba mizigo na basi la abiria ilitokea Jumanne asubuhi karibu na daraja la Mto Manyame kwenye Barabara ya Seke, inayounganisha mji mkuu wa Harare na mji wa Chitungwiza, msemaji wa polisi Paul Nyathi alisema katika taarifa.
Abiria waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini, huku maafisa wakihofia kuwa huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.
Walioshuhudia walisema watoto wawili na wapita njia wawili, ambao waligongwa na lori hilo kabla ya kugonga basi, ni miongoni mwa waliofariki.