MICHEZO
1 dk kusoma
WAFCON 2024: Wenyeji Morocco kukabiliana na Nigeria fainali
Ghana na Afrika Kusini watapambania nafasi ya tatu mjini Casablanca siku ya Ijumaa huku fainali ikichezwa Rabat siku ya Jumamosi.
WAFCON 2024: Wenyeji Morocco kukabiliana na Nigeria fainali
Nigeria iliwafunga Afrika Kusini 2-1 katika nusu fainali ya WAFCON Jumanne. / CAF
23 Julai 2025

Morocco na Nigeria watakabiliana Jumamosi kuamua mshindi wa mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wanawake baada ya timu zote kufuzu kwenye mechi zao za nusu fainali siku ya Jumanne.

Wenyeji Morocco waliwafunga Ghana kupitia penati katika uwanja wa Stade Olympique huko Rabat huku Nigeria wakiwafungisha virago mabingwa watetezi Afrika Kusini kwa magoli 2-1 mjini Casablanca.

Goli la Michelle Alozie ndiyo lilokuwa la ushindi kwa timu ya Nigeria dakika nne kabla ya muda ulioratibiwa kumalizika.

Ghana hawakuwa wamepewa nafasi kubwa dhidi ya Morocco, ambao walikuwa wanaungwa mkono na mashabiki wa nyumbani, lakini Stella Nyameke aliipatia timu ya Ghana goli la utangulizi katika dakika ya 26.

Morocco ilisawazisha katika kipindi cha pili kupitia bao la Sakina Ouzraoui na kushinda kupitia penati magoli 4-2 baada ya muda wa ziada. Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu itakuwa kati ya Ghana na Afrika Kusini jijini Casablanca Ijumaa huku fainali ikichezwa siku ya Jumamosi.

Mechi hizo zilikuwa zimeratibiwa kuchezwa mwaka uliopita lakini zikaahirishwa kwa sababu zilikuwa wakati mmoja na michezo ya Olimpiki ya Paris.

Mashindano mengine ya fainali za mataifa ya Afrika kwa wanawake yatafanyika tena Morocco mwakani.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us