AFRIKA
2 dk kusoma
Watoto 80,000 wako katika hatari kubwa ya kipindupindu Afrika Magharibi na Kati: UNICEF
Mlipuko wa kipindupindu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Nigeria umeibua tishio la maambukizi hayo kuenea nje ya mipaka, shirika la Umoja wa Mataifa limesema
Watoto 80,000 wako katika hatari kubwa ya kipindupindu Afrika Magharibi na Kati: UNICEF
31 Julai 2025

Watoto takriban 80,000 wako katika hatari ya kuugua kipindupindu huku msimu wa mvua ukianza katika maeneo ya Afrika Magharibi na Kati, shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto UNICEF limesema siku ya Jumatano.

Katika taarifa, shirika hilo limesema kuwa milipuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Nigeria yanasababisha hatari ya mlipuko wa kipindupindu kuenea, na kusababisha hatari ya kuvuka mipaka hadi katika nchi jirani.

Huko Congo, eneo lililoathirika zaidi, maafisa wa afya wameripoti maambukizi 38,000 mwezi Julai na vifo 951, huku watoto walio na umri ya chini ya miaka mitano wakiwa ni asilimia 25.6 ya maambukizi, kulingana na UNICEF.

Mataifa mengine ambayo yanakabiliana na tatizo la kipindupindu ni pamoja na Chad, Jamhuri ya Congo, Ghana, Cote d’Ivoire na Togo.

UNICEF inasema kuna umuhimu wa kuimarisha juhudi za kuhakikisha kuwa wanakabiliana na hali ili ugonjwa usienee katika kanda nzima.

“Mvua kubwa, mafuriko na watu kuondolewa katika makazi yao yote hayo yamesababisha maambukizi ya kipindupindu zaidi na kuweka maisha ya watoto wengi hatarini,” amesema mkurugenzi wa kanda ya Afrika Magharibi na Kati wa UNICEF Gilles Fagninou.

“Tayari kuna tatizo kubwa la maji safi na mazingira, hatua za haraka zinahitajika. Hili ni suala la maisha ya watu,” Fagninou aliongeza.

Watoto, hasa wale walio chini ya umri wa miaka mitano, wako katika hali mbaya zaidi ya kupata kipindupindu kutokana na masuala kama mazingira yasiyo safi, kukosekana kwa maji safi, na kuwa na tatizo la kuharisha.

Kuimarisha juhudi za kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu hali imeimarishwa kote kwenye kanda katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, na kwa hali hii kanda ya Afrika Magharibi na Kati ya UNICEF inahitaji dola milioni 20 kufanikisha misaada muhimu kwa watu.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us