Ushawahi kuhisi hali y akiua kuwaka moto, au gesi kali inataka kupanda kukufanya uteuke ovyo na wakati mwingine ukijaribu kuteuka unaweza kuambatana na majimaji ya moto?
Madaktari wanasema hiki kiungulia ni kitu cha kawaida na japo kinakera, hakina madhara makubwa na mara nyingi hutokea baada ya kula.
Inatokea wakati asidi ya tumbo inapita tena kwenye umio (mrija unaounganisha mdomo wako na tumbo lako). Hii ikitokea asidi inaweza inakera au kuchoma utando wa umio, na kusababisha usumbufu na kwa hali mbaya zaidi unaweza kufanya vidonda.
Baadhi ya sababu za Kiungulia
Kiungulia mara nyingi kinasababishwa na chakula. Imma aina ya chakula au namna ulivyukula au unachoanya punde baada ya kula.
Unaweza kupata kiungulia ukila chakula kingi kupita kiasi, chakula cha mafuta mengi, au ukilala punde tu baada ya kula.
Pia unaweza kuathirika kwa kula vyakula vyenye asidi au viungo vingi. Kunywa kafeini, pombe au vinywaji vya kaboni au vyenye gesi. Unaweza pia kupata kiungulia kutokana na kuvuta sigara.
Wataalamu wanasema pia uzito mkubwa wa mwili au wanawake waa wazito wanapata sana kiungulia. Lakini pi aunaweza kupata kutokana nautumiaji wa dawa fulani (kama vile dawa za kutuliza maumivu au shinikizo la damu).
Kuepuka Kiungulia
Kula milo midogo - Milo mikubwa huweka shinikizo kwenye tumbo lako na kuongeza nafasi ya kupanda au kuteuka asidi.
Epuka vyakula vinavyochochea - Vichochezi vikubwa kawaida ni pamoja na nyanya (tomato), chokoleti, matunda ya machungwa, vitunguu, na vyakula vya kukaanga.
Usilale baada ya kula - Subiri angalau masaa 2-3 kabla ya kulala au kujilaza.
Inua kichwa Chako Unapolala - Mteremko mdogo unaweza kuzuia kupanda gesi usiku.
Dumisha Uzito wa Afya - Uzito wa ziada unaweza kusukuma tumbo lako na kusababisha asidi kuongezeka.
Vaa nguo nyepesi - Nguo zenye kubana kiunoni zinaweza kukandamiza tumbo lako.
Acha kuvuta Sigara - Inadhoofisha misuli inayoweka asidi kwenye tumbo lako.
Punguza Pombe na vinywaji vya Kafeini - Zote mbili zinaweza kudumaza misuli inayofunga mlango wa tumbo, kuruhusu asidi kupanda juu.