Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa vita nchini Ukraine na kuzitaka Kiev na Moscow kushiriki katika "mashauriano yenye matokeo" wakati wa duru mpya ya mazungumzo ya amani yanayofanyika Istanbul.
"Tunapaswa kumaliza vita hivi vya umwagaji damu haraka iwezekanavyo," Fidan alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Istanbul siku ya Jumatano kabla ya mazungumzo, ambayo yatakuwa duru ya tatu ya mazungumzo mapya kati ya pande hizo mbili tangu mwezi Mei.
Juhudi za kidiplomasia za Ankara
Fidan alisisitiza kuwa Uturuki imekuwa na jukumu kubwa la kidiplomasia tangu mwanzo wa mzozo, na kuongeza: "Uturuki imefanya juhudi kubwa chini ya uongozi wa Rais Erdogan tangu mwanzo wa mzozo huu."
Alisema lengo la Ankara ni pande husika kuendeleza mazungumzo ya awali na kuzingatia hatua madhubuti za kusonga mbele.
"Lengo letu ni kwamba pande zote zitakuwa na mashauriano yenye mwelekeo wa matokeo juu ya makubaliano hayo," alisema, akimaanisha nyaraka zilizobadilishwa katika duru za awali za mazungumzo ambayo yaliweka msingi wa mapendekezo ya kusitisha mapigano na makubaliano ya masula ya kibinadamu.
"Lengo kuu," aliongeza, "ni kujenga amani kupitia usitishaji mapigano."
Maoni hayo yanakuja wakati wajumbe wa Urusi na Ukraine wakianza majadiliano yanayotarajiwa kulenga kupanua mabadilishano ya wafungwa, na kujenga mazigira ya kufunguliwa kwa njia za kibinadamu, na kuweka msingi wa kukomesha vita.
Duru ya mwisho ya mazungumzo mwezi Juni ilisababisha makubaliano ya kihistoria juu ya kurejesha miili ya wanajeshi waliokufa na kuwapa kipaumbele wafungwa wa vita waliojeruhiwa vibaya.