AFRIKA
1 dk kusoma
Osimhen arudi rasmi Galatasaray baada ya kumalizana na Napoli
Hatua hiyo inakuja baada ya mazungumzo ya muda mrefu na Napoli, baada ya nyota huyo Mnigeria kuichezea Galatasaray kwa mkopo, msimu uliopita.
Osimhen arudi rasmi Galatasaray baada ya kumalizana na Napoli
Nyota wa Nigeria, Victor Osimhen./TRT Spor
31 Julai 2025

Klabu ya Galatasaray imefikia makubaliano ya kumsajili mazima nyota wa Nigeria Victor Osimhen kutokea knali ya Napoli ya nchini Italia.

Osimhen, ambaye alisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Galatasaray, aliwasili katika uwanja wa ndege wa Atatürk jijini Istanbul, akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa klabu ya Galatasaray, Abdullah Kavukcu.

“Sina namna ya kuelezea furaha hii. Ni raha iiyoje kuwepo hapa. Tazama huu umati unavyoisindikiza ndege. Niko nyumbani. Hapa ndipo napostahili kuwepo,” alisema Osimhen wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Mfumania nyavu huyo mwenye umri wa miaka 26, anategemewa kufanyiwa vipimo vya afya Julai 31, kabla ya kusaini mkataba na klabu ya Galatasaray.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us