AFRIKA
1 dk kusoma
Wapiganaji wa RSF Sudan wadai kudhibiti mpaka muhimu na Misri, Libya, huku jeshi likiondoka
Jeshi la Sudan limethibitisha kuondoka katika eneo hilo la mpakani kama sehemu ya ‘mpango wa kuandaa ulinzi’
Wapiganaji wa RSF Sudan wadai kudhibiti mpaka muhimu na Misri, Libya, huku jeshi likiondoka
Sudan
11 Juni 2025

Siku ya Jumatano wapiganaji wa Sudan wa Rapid Support Forces (RSF) wamedai kuwa wamechukwua udhibiti wa eneo la mpakani na Misri na Libya, huku jeshi la Sudan likiondoka eneo hilo.

Msemaji wa RSF amesema kuwa kundi hilo la waasi limedhibiti eneo la kimkakati la "Pembe tatu", njia ya makutano inayounganisha Sudan, Libya, na Misri, baada ya makabiliano na vikosi vya jeshi.

Alidai kuwa wamewaua wanajeshi kadhaa wa Sudan pamoja na kuharibu silaha zao wakati wa mapigano hayo.

Jeshi lilithibitisha kuwa vikosi vyake viliondoka kutoka eneo hilo la mpakani kama sehemu ya ‘mpango wa kuandaa ulinzi na kukabili upinzani’

Jeshi la Sudan limemlaumu kamanda wa kijeshi wa Libya Khalifa Haftar kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa RSF, akisema kuwa “ni jambo baya sana” na “ukiukwaji wa sheria ya kimataifa.”

Wapiganaji wa RSF na jeshi wamekuwa wakipigana tangu Aprili 2023, jambo lililosababisha vifo vya maelfu ya watu na hali mbaya zaidi kwa watu wa Sudan kote duniani.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us