ULIMWENGU
7 dk kusoma
Jinsi upofu wa kimkakati ulidhihirisha udhaifu wa Iran
Mashambulio ya anga ya Israeli yalifichua zaidi ya udhaifu wa kijeshi; yalifichua kushindwa kwa mfumo mzima wa Iran katika uwezo wake wa kufikiria kimkakati katika ulimwengu ulioingiliana.
Jinsi upofu wa kimkakati ulidhihirisha udhaifu wa Iran
Bendera ya Irani inaning'inia juu ya jengo lililoharibiwa na shambulio huko Tehran. / AP
22 Julai 2025

Mnamo Juni 2025, mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Iran yalifichua sio tu miundo mbinu bali pia dosari za kina za kimuundo ndani ya chombo cha kimkakati cha kufanya maamuzi cha Iran.

Uchokozi wa Israel - sehemu ya muundo mpana wa vitendo vya kijeshi vya kuvuka mipaka, ilionyesha tena nia ya Tel Aviv kuzidsiha uchokozi bila makubaliano ya kikanda.

Mzozo huo ulifichua kushindwa kwa uanishaji, kuchelewa kwa majibu kutoka kwa vituo vya kutoa amri, na kuvuruga mtiririko wa habari, ni ishara tosha ya kuwa haikuwa tayari kwa shambulio ya hali ya juu.

Ingawa mambo ya ndani kama vile mwingiliano wa mamlaka kati ya huduma za kijasusi, uratibu hafifu kati ya kiraia na taasisi za usalama, na kuongezeka kwa ushindani baina ya mashirika yalitoa dhima, masuala haya ya kiutendaji yanaelekeza kwenye sababu ya msingi zaidi: Usanifu wa kiakili wa Iran, ambao bado umefungwa, hauelekei moja kwa moja, na umebanwa kiitikadi.

Mshtuko uliokumba Iran haukutokana tu na kutojitayarisha kijeshi bali katika upofu wa kimkakati.

Fikra za kimkakati katika mzunguko uliofungwa

Kutengwa kwa maarifa (au kutengwa kwa kimaudhui) kunaweza kufafanuliwa kama mwelekeo wa taifa kuunda na kutathmini maarifa kwa kutumia tu mifumo yake ya kiitikadi, kitaasisi na kitamaduni, huku likiepuka kwa makusudi vyanzo vya habari kutoka nje. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikiwakilisha kwa muda mrefu mtazamo wa aina hii.

Utawala hujihusisha na watendaji wanaowiana na mfumo wake wa kiitikadi lakini huepuka mwingiliano wa kitaasisi wenye maana na nyanja za kimataifa za kielimu, kimkakati, au maarifa ya kiteknolojia.

Hali hii inadhoofisha uwezo wa Irani wa kuunda hali mbadala, kuchambua tabia ya adui, na kujirekebisha kimkakati. Katika mazingira kama haya, ambapo wahusika watendaji ni wa fikra moja na bila kuunganishwa kiutendaji, fikra za kimkakati huwa za mzunguko na za kujirejelea.

Kwa upande wa Iran, hii inajidhihirisha katika kuegemea kwa dhana zisizobadilika na tafsiri ngumu za uzoefu wa zamani wakati wa kutathmini vitisho vya kisasa.

Iwe ni shambulio la mtandaoni, vuguvugu la maandamano, usumbufu wa kiuchumi, au uvujaji wa taarifa za kijasusi, majibu ya mara moja mara nyingi yanahusisha kuhusisha Israel au Marekani kuwajibika, bila kujali ushahidi ulioko.

Maafisa wa Irani wameelezea janga la COVID-19 kama silaha ya kibaolojia ya Marekani na Israeli, na wameonyesha majukwaa kama TikTok kama zana za ushawishi wa Kizayuni. Fikra kama hizi zinaonyesha jinsi mtazamo wa tishio la Irani unavyosalia kuwa mfumo wa seti finyu ya violezo vya kiitikadi na kihistoria.

Kwa ndani, utoaji wa maarifa unakabiliwa na uangalizi mkali wa kiitikadi. Vyuo vikuu, waunda sera, vyombo vya habari na kundi la wataalamu hawaruhusiwi kufanya kazi kwa uhuru. Uchanganuzi unaotofautiana na mfumo mkuu wa kiitikadi hukandamizwa au kutengwa kimfumo.

Hii imeruhusu kundi fulani la wasomi wanaohusishwa na utawala, ikiwa ni pamoja na taasisi za utafiti zinazofadhiliwa na serikali na mitandao ya wasomi waaminifu, kuhodhi mazungumzo ya usalama, ambayo hatua kwa hatua hayawezi kutofautishwa na mtazamo rasmi wa tishio la serikali.

Kwa hivyo, michakato ya kijasusi inashindwa kuona hali mbadala, mitazamo muhimu, au mbinu tofauti za kielimu.

Uchambuzi wa usalama na sera za kigeni unafanywa na kundi finyu lililochaguliwa hasa kwa misingi ya uaminifu wa kisiasa, na hivyo kusababisha utamaduni wa kimkakati wenye uwezo mdogo wa kuona mbele na miundo thabiti ya kufanya maamuzi.

Kukandamiza utofauti wa kiakili kwa njia hii kunapunguza sio tu nguvu ya kiakili ya mfumo lakini pia uwezo wake wa kubadilika kimkakati.

Kufungwa kwa utofauti wa maono ya Iran hakukomei kwa nadharia au utamaduni wa kitaasisi; inaenea hadi katika mazoezi ya kijeshi. Wakati Iran mara kwa mara hufanya mazoezi machache kati ya mataifa mawilii na washirika waliochaguliwa, nchi haishiriki (au haiwezi kushiriki) katika ushirikiano endelevu wa kijeshi wa kimataifa, na hivyo kupoteza fursa za utaratibu wa kuchunguza mafundisho ya kupambana, mbinu za pamoja za uendeshaji, na majibu ya vitisho vinavyoibuka.

Mazoezi kama haya sio maonyesho ya nguvu tu. Zinafanya kazi kama maabara za maono tofauti za kukabiliana, kulinganisha, na kujifunza.

Kwa kutoshiriki, Iran inaendelea kufanya mazoezi ya mifano ya zamani iliyotokana na uzoefu wake wa ndani wa mapinduzi na zama za vita. Mafundisho kama vile "ulinzi usiolinganishwa, na "uzuiaji wa balestiki," uliorithiwa kutoka kwa Vita vya Iran-Iraq, yanasalia kuwa kiini cha mawazo yake ya kimkakati.

Wakati huo huo, vita vya kisasa vimebadilika kuwa operesheni za vikoa vingi vinavyoungwa mkono na mifumo ya amri inayotegemea akili mnemba (AI), uwezo wa kulenga shabaha kwa usahihi, na ujumuishaji wa habari wa wakati halisi.

Kwa kukosa kujihusisha na ubunifu huu, Iran polepole inapoteza muono wa kimkakati na inaelekea kutafsiri mienendo ya kisasa ya usalama kupitia dhana zilizopitwa na wakati, na kufanya majibu yake kuzidi kutabirika.

Mkakati wa ushiriki wa nje wa Iran unaimarisha zaidi hali hii ya kiakili.

Majadiliano ya kidiplomasia, hasa na mataifa ya Magharibi au pinzani, hayachukuliwi kama fursa za kuelewana au majaribio ya hali ilivyo. Badala yake, mara nyingi hutumika kama majukwaa ya kukadiria masimulizi ya kiitikadi na kukuza uhalali wa utawala mbele ya hadhira ya raia. Tabia hii haizui tu mazungumzo ya hali ya juu bali pia mtiririko wa taarifa zisizo rasmi na uchunguzi ambao kwa kawaida huboresha uchanganuzi wa kimkakati.

Uwezo wa kutathmini nia kwa usahihi, mitazamo, na kujua uwezo wa kujua udhaifu wa wahasimu unadhoofika, kwani mawasiliano huwa ya mwelekeo mmoja. Kwa hivyo, uchanganuzi wa kimkakati unazidi kujitenga na kubadilisha hali halisi za ulimwengu na kuegemea zaidi katika njia za kiitikadi zilizowekwa mapema.

Hatari ya kutobadilisha mkakati

Mojawapo ya matokeo muhimu zaidi ya kufungwa huku kwa maono mbadala ni kukataa kimakusudi kwa serikali kujihusisha na waunda sera, taasisi, au mifumo ya maarifa ambayo inatofautiana na mpangilio wake wa kiitikadi.

Hii inatumika sio tu kwa sauti za upinzani lakini pia kwa mitazamo inayoweza kuwa muhimu.

Ushirikiano wa kielimu, ubadilishanaji wa kitaasisi, na ushiriki katika mabaraza ya kimkakati ya kimataifa hudhibitiwa kwa uthabiti au kukabidhiwa kwa wawakilishi ambao wanasisitiza tu masimulizi rasmi ya serikali.

Taasisi ya kisiasa ya Irani inaamini kuwa maarifa na uchambuzi wa kimkakati wa nje hauleti hatari ya usimamizi tu, bali pia tishio la kupenya kiitikadi. Matokeo yake, uzalishaji wa maarifa na mzunguko umeundwa kwa njia iliyodhibitiwa sana na ya ndani.

Kwa mtazamo wa serikali, mkabala huu unajumuisha chaguo la kimantiki linalowiana na hitaji lake la uwiano wa kiitikadi na utulivu wa kimfumo.

Hata hivyo, uteuzi huu huiingiza Iran ndani ya ulimwengu finyu wa matukio machache tu kwa washirika inaowaona kuwa wa urafiki au wanaolingana. Katika mazingira kama haya, mfiduo wa mabadiliko ya kimafundisho, kiteknolojia na kimkakati yanayotokea nje ya mipaka yake inabaki kuwa mdogo.

Utamaduni wa kimkakati usio na utofauti na uendeshaji wa habari iliyochujwa, baada ya muda, itazalisha mbinu za kufanya maamuzi ambazo zimefungwa, ngumu, na hatari zaidi kwa mikakati.

Mzozo wa Juni 2025, kwa hivyo, lazima uonekane sio tu kama mtihani wa utayari wa kijeshi wa Iran, lakini pia kama kiashiria pana cha kupungua kwa uwezo wake wa muono wa kimkakati.

Mgogoro huo ulifichua mapungufu makubwa ya uratibu, uzembe wa majibu ya kitaasisi, na kutoweza kutanguliza vitisho chini ya shinikizo. Matatizo haya hayawezi kuelezewa tu na uzembe wa ukiritimba au migogoro ya kijasusi.

Kwa undani, kujitenga kwa Iran, kunakojulikana kwa kutoamini maarifa ya nje na kuegemea kupita kiasi kwa utaalamu wa ndani unaotegemea uaminifu, kulidhoofisha kwa kiasi kikubwa uwezo wake wa kukadiria na kulipiza kwa haraka.

Kwa kukosekana kwa mawazo ya kimkakati ya wazi zaidi na ya kuunganisha, hatari ya kushindwa kwa siku zijazo, uwezekano wa kupata hasara ya gharama kubwa zaidi, inabakia kuwa juu.

Maoni yaliyotolewa na mwandishi si lazima yaakisi maoni na sera za uhariri za TRT Afrika.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us