AFRIKA
2 DK KUSOMA
Rwanda: hakuna kipengee cha kurejesha fedha za UK
Serikali ya Rwanda imesema hakuna kifungu cha mkataba kinachoilazimisha kurejesha pesa za Uingereza kwa mpango wa uhamisho ulioshindwa wa wahamiaji.
Rwanda: hakuna kipengee cha kurejesha fedha za UK
Takriban waomba hifadhi 24,000 walipaswa kuhamishiwa Rwanda, huku Uingereza ikiripotiwa kuilipa Rwanda takriban dola milioni 176 kwa uhamisho huo Juni 2022. / Picha: TRT Afrika / Others
10 Julai 2024

Serikali ya Rwanda ilisema Jumanne kwamba mkataba wake wenye utata wa wahamiaji na Uingereza haukuweka wazi kurejeshwa kwa fedha, kufuatia uamuzi wa serikali mpya ya Uingereza kufuta mpango huo.

"Mkataba tuliotia saini haukuweka bayana kwamba tunapaswa kurejesha pesa. Hili liwe wazi, kulipa pesa hizo kamwe haikuwa sehemu ya makubaliano," naibu msemaji wa serikali Alain Mukuralinda aliambia televisheni ya taifa.

Takriban waomba hifadhi 24,000 walitakiwa kuhamishiwa Rwanda, huku Uingereza ikiripotiwa kuilipa Rwanda takriban dola milioni 176 kwa uhamisho huo Juni 2022.

Uingereza pia ilipaswa kulipa $15,100 kwa kila mtu wa ziada aliyepelekwa Rwanda.

Uhamiaji halisi

Uingereza inaruhusu maombi ya hifadhi, aina ya ulinzi ambayo huwezesha mtu kusalia nchini bila kufukuzwa.

Uingereza inatarajia kupunguza idadi ya wanaotafuta hifadhi hadi chini ya 100,000 kila mwaka. Serikali ilisema kuwa mnamo 2022 pekee, kulikuwa na wahamiaji 606,000.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us