26 Julai 2025
Jeshi la Israel limevamia meli ya misaada ya Handala iliyokuwa inaelekea Gaza, ikiwa na watu 21 ndani, muda mfupi tu baada ya meli hiyo kutoa ujumbe wa tahadhari ya kuvamiwa.
Matangazo ya moja kwa moja yameonyesha wanaharakati hao wakiwa wamekaa siku ya Jumamosi, wakishikilia vichwa vyao, huku wanajeshi wakiiongoza meli hiyo.
Video tatu vya tukio hilo, zilizoonyesha tukio hilo moja kwa moja, baadae zilisitishwa.