ULIMWENGU
1 dk kusoma
Viongozi wa dunia wafurahishwa na hatua ya Ufaransa kulitambua Taifa la Palestina
Saudi Arabia nayo imelipongeza tangazo la Macron na kutaka nchi nyengine kufuata mfano huo.
Viongozi wa dunia wafurahishwa na hatua ya Ufaransa kulitambua Taifa la Palestina
Ufaransa kulitambua Taifa la Palestina katika Umoja wa Mataifa ifikapo September, amesema Macron / AFP
25 Julai 2025

Viongozi mbalimbali wa dunia wamefurahishwa na tangazo la Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwamba nchi yake italitambua taifa la Palestina ifikapo mwezi September, ikisema hatua hiyo ni muhimu katika kufikia amani ya Mashariki ya Kati.

“Nimefurahishwa na tangazo la Rais Macron kwamba Ufaransa itaitambua Palestina mwezi September,” amesema Waziri Mkuu wa Irish Simon Harris kupitia X.

Nae Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez ameunga mkono uamuzi huo wa Ufaransa, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa njia ya majadiliano.

“Naikaribisha Ufaransa na Uhispania na nchi nyengine za Ulaya katika kulitambua taifa la Palestina, amesema kupitia X.

“Kwa pamoja tujaribu kulinda kile Netanyahu anachojaribu kukiharibu. Suluhu ya mataifa mawili ndio suluhu pekee,” ameongeza.

Waziri Kiongozi wa Uskochi John Swinney pia ametilia mkazo, na kuitaka serikali ya Uingereza kuchukua hatua kama hiyo.

Saudi Arabia nayo imelipongeza tangazo la Macron na kutaka nchi nyengine kufuata mfano huo.

“Falme inapongeza uamuzi wa kihistoria, ambao inathibitisha makubaliano ya jumuia ya kimataifa katika haki ya watu wa Palestina ya kuwa na taifa linalojitegemea,” imesema taarifa ya wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us