ULIMWENGU
3 dk kusoma
Marekani kuondoka UNESCO
Kwa mujibu wa serikali ya Rais Donald Trump hatua hiyo inafuatia uamuzi wa UNESCO wa kukubali Palestina kama nchi mwanachama ni kinyume na sera ya Marekani.
Marekani kuondoka UNESCO
Marekani kujiondoa kwa UNESCO baada ya shirika hilo kuitambua Palestina/ Picha: AA
25 Julai 2025

Marekani imetangaza kuwa itajiondoa kutoka wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambapo imekuwa mdau mkubwa. UNESCO ilianzishwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia ili kukuza amani kupitia ushirikiano wa kimataifa katika Elimu, Sayansi na Utamaduni.

Jukumu lake kuu ni kuhifadhi tamaduni na maneno muhimu. 

Msemaji wa Ikulu ya White House Anna Kelly alisema UNESCO "inaunga mkono sababu zilizoamka, za kitamaduni na kijamii ambazo haziendani kabisa na sera ambazo Wamarekani walipigia kura."

Kwa mujibu wa serikali ya Rais Donald Trump hatua hiyo inafuatia uamuzi wa UNESCO wa kukubali Palestina kama nchi mwanachama ni kinyume na sera ya Marekani.

Marekani imedai Shirika hilo linaangazia maendeleo ya kimataifa ilhali Marekani sasa ina msingi wa sera za kuzingatia Marekani kwanza. 

Marekani imejulikana kuiunga mkono Israeli katika vita yake dhidi ya Palestina. UNESCO imejibu kwa kusema kuwa jukumu lake ni kukaribisha nchi zote kuwa wananchama na kuendeleza ajenda ya kuhifadhi tamaduni. 

UNESCO imesema, sababu zilizotolewa na Marekani kujiondoa katika Shirika hilo ni sawa na zile zilizotolewa miaka saba iliyopita wakati Marekani ikiwa chini ya Rais Trump.

Lakini nchi hiyo, ilirudisha tena uanachama wake ilipokuwa chini ya Rais Joe Biden. Inasema madai haya pia yanakinzana na uhalisia wa juhudi za UNESCO, hasa katika uwanja wa elimu ya mauaji dhidi ya wayahudi na mapambano dhidi ya chuki dhidi ya Wayahudi. 

“ Uamuzi huu unakinzana na kanuni za kimsingi za ushirikiano wa pande nyingi, na unaweza kuathiri kwanza kabisa washirika wetu wengi nchini Marekani—jumuiya zinazotafuta uandishi wa tovuti kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia, hadhi ya Jiji Ubunifu, na Wenyeviti wa Vyuo Vikuu,” Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCo alisema katika taarifa.

UNESCO inasema katika miaka ya hivi karibuni, imefanya mageuzi makubwa ya kimuundo na kubadilisha vyanzo vya ufadhili na kuacha kutegema Marekani kama ilivyokuwa awali. 

Ufadhili kwa UNESCO

Takwimu za UNESCO zinaonyesha kuwa hadi sasa Marekani imeongoza kwa mchango wa dola milioni 156, 698, 000 ikifuatwa kwa karibu na China  ambayo inachangia dola milioni 132,119,000 na ya tatu ni Japan ambayo inachangia dola milioni 91, 700,000. 

Shirika hili pia linapata ufadhili kutoka Benki ya Dunia, na mataifa mengine kama vile Canada, Brazil, Ufaransa na Ujerumani. 

Hata hivyo, UNESCO inasema kuwa kwa sasa haitegemei Marekani kwa kiasi kikubwa Marekani, baada ya nchi hiyo kupunguza mwelekeo wa mchango wake wa kifedha kwa Shirika hilo tangu mwaka 2018.

“ Leo, Shirika linalindwa vyema katika masuala ya kifedha,” Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCo alliongezea.

Kwa mujibu wa UNESCO, mchango wa Marekani katika bajeti yake ni asilimia nane tu ikilinganishwa na mchango wa Merkani wa asilimia 40 kwa baadhi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa. UNESCO inasema tangu 2018 imepata uthabiti wa idadi kubwa ya nchi wengine wanachama na wachangiaji binafsi.

Barani Afrika UNESCO imeteua maeneo 147 ya Urithi wa Dunia barani Afrika katika nchi 46. Marekani itaondoka UNESCO mwisho wa 2026.


Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us