AFRIKA
1 dk kusoma
Mlima Kilimanjaro wang'ara kati ya maeneo ya kuvutia kwa picha ulimwenguni
Jumla ya wapandaji 50,000 hukwea mlima huo kila mwaka, huku ukivutia watumiaji wa mitandao zaidi ya milioni 5.5 kila mwaka.
Mlima Kilimanjaro wang'ara kati ya maeneo ya kuvutia kwa picha ulimwenguni
Mlima Kilimanjaro mmoja ya vivutio maarufu duniani./Picha: Wengine / Others
30 Aprili 2025

Mlima Kilimanjaro umeshika nafasi ya pili katika kipengele cha maeneo yenye kuvutia zaidi kwa picha duniani, kulingana na utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na taasisi ya Heepsy.

Mlima huo, ambao unapatikana nchini Tanzania, umeshika nafasi ya pili nyuma ya jengo la Burj Khalifa la Dubai na pia kuushinda mnara wa Eiffel unaopatikana nchini Ufaransa.

Jumla ya wapandaji 50,000 hukwea mlima huo kila mwaka, huku ukivutia watumiaji wa mitandao zaidi ya milioni 5.5 kila mwaka.

Nafasi ya nne imechukuliwa na mnara wa saa wa jijini London, maarufu kama ‘Big Ben’, wakati visiwa vya Galápagos vya nchini Ecuador vikiwa katika nafasi ya tano.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us