27 Aprili 2025
Ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikielekea Dar es Salaam kutoka Nairobi ililazimika kurudi kutua uwanja wa Jomo Kenyatta baada ya tukio la kiafya, kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na shirika hilo kwenye mtandao wa X.
Taarifa hiyo ilisema kuwa maafisa wa afya na walipokea ndege hiyo huku wakiimarisha itifaki za kiafya kudhibiti tukio hilo.
Baada ya saa mbili ya kusibiri ndege hiyo iliruhusiwa kuendelea na safari yake kwenda Dar es Salaam.
‘‘Usalama na ustawi wa wageni na wafanyakazi wetu unasalia kuwa kipaumbele chetu cha juu zaidi’’ ilisema taarifa hiyo.
Japo kumekuwa na uvumi katika baadhi iya vyombo vya habari, Kenya Airways haikutaja sababu ya dharura hiyo.