AFRIKA
1 dk kusoma
Biya atangaza uchaguzi wa urais Cameroon kufanyika Oktoba
Rais Paul Biya, kiongozi wa nchi mwenye umri mkubwa zaidi duniani akiwa na miaka 92, hajasema kama ana nia ya kugombea kwa muhula mwingine.
Biya atangaza uchaguzi wa urais Cameroon kufanyika Oktoba
Paul Biya amekuwa Rais wa Cameroon tangu 1982./ Reuters
11 Julai 2025

Cameroon itafanya uchaguzi wake wa urais tarehe 12 Oktoba, amri iliyosainiwa na Rais wa taifa hilo la Afrika ya Kati Paul Biya ilionesha siku ya Ijumaa.

Uchaguzi huo utaamua nani ataongoza taifa hilo la uzalishaji kakao na mafuta lenye idadai ya watu karibu milioni 30 katika kipindi cha miaka saba ijayo.

Wagombea wa urais wanatakiwa kuwasilisha maombi yao siku 10 baada ya baraza la uchaguzi kuundwa, kama kanuni ya uchaguzi inavyotaka.

Biya, kiongozi wa nchi mwenye umri mkubwa zaidi duniani akiwa na miaka 92, aliingia madarakani miongo minne iliyopita mwaka 1982. Hajasema kama ana nia ya kugombea muhula mwingine tena.

Alishinda mwaka 2018 na asilimia 71.28 ya kura, kulingana na matokeo rasmi, ingawa upinzani ulidai kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi huo.

Mabadiliko ya katiba 2008 yaliondowa ukomo wa mihula ya rais, kumpa nafasi yeye kugombea bila pingamizi.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us