AFRIKA
2 DK KUSOMA
Raia 206 wa Tanzania waliokuwa Sudan wawasili salama
Tanzania imepokea raia wake katika uwanja wa ndege wa Dar es Saalam baada ya kusafiri kwa siku kadhaa kutoka Sudan ambako mapigano makali yanaendelea kati ya Jeshi la nchi hiyo na askari kutoka Jeshi saidizi.
Raia 206 wa Tanzania waliokuwa Sudan wawasili salama
Raia wa Tanzania wa wasili kutoka Sudan / Others
27 Aprili 2023

Hii leo Serikali ya Tanzania kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Stergomena Tax akiungana na familia za ndugu wa watanzania waliokuwa Sudan wamewapokea nyumbani raia wake 206 waliowasili na ndege ya serikali Air Tanzania.

Katika kundi hilo la watanzania lililowasili baadhi yao ni wanafunzi waliokuwa wakisoma nchini Sudan.

Hata hivyo waziri huyo amebainisha ugumu unaoendelea kujitokea wa kuwapata raia wake wote waliokwama Sudan kwani baadhi walikuwa hawaja jisajili.

"Changamoto iliyopo Watanzania wengi hawajajisajili kwenye ubalozi wetu, ndiyo maana mnaona siku ya kwanza nilisema raia walioko tayari 200 lakini leo idadi imeongezeka, kuwapata imekuwa shida," amesema Dk Stergomena

Hata hivyo Tanzania imebainisha kuwa bado kuna raia wengine ambao wamesalia nchini humo huku akisisitiza umuhimu wa kujisajili unapokuwa ughaibuni.

Mzozo nchini Sudan bado unaendelea na idadi kubwa ya watu wame uawa na kujeruhiwa tangu Aprili 15 wakati mzozo ulipozuka katika mji mkuu Khartoum na miji mingine kati ya Jeshi la Sudan na RSF, kundi ambalo lilikuwa limetangazwa kuwa kundi la waasi.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us