ULIMWENGU
1 DK KUSOMA
Israeli yaua zaidi ya watu 800 ndani ya wiki moja nchini Lebanon
Mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza yameingia siku ya 359, yakiwa yameua Wapalestina 41,595. Zaidi ya watu 800 wamepoteza maisha toka kuanza kwa mashambulizi ya Israeli katika maeneo kadhaa ya Lebanon.
Israeli yaua zaidi ya watu 800 ndani ya wiki moja nchini Lebanon
Kulingana na takwimu za shirika la habari la Anadolu, watu 1,640 wameuwawa na wengine 8,408 wamejeruhiwa nchini Lebanon kuanzia Oktoba mwaka jana. /Picha: AA   / Others
29 Septemba 2024

Watu 816, wakiwemo wanawake na watoto wameuwawa na wengine 2,507 wamejeruhiwa kupitia mashambulizi ya anga ya Israeli nchini Lebanon kuanzia Septemba 23, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya ya Lebanon.

Jeshi la Israeli limeendelea kuongeza mashambulizi yake dhidi ya kile kinachokiita "Hezbollah", ikiwa ni ongezeko la mwaka mmoja wa vita vya kuvuka mpaka kati ya pande hizo mbili tangu Oktoba mwaka jana.

Kulingana na takwimu zilizoandaliwa na Shirika la Habari la Anadolu, watu 1,640 wameuwawa na wengine 8,408 wakijeruhiwa.

Idadi hiyo huenda ikaongezeka huku jeshi la Israeli likiendelea kufanya mashambulizi ya anga katika maeneo mbalimbali nchini Lebanon.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us