ULIMWENGU
1 dk kusoma
Papa Francis azikwa: Siku tisa za Novendiale zaanza
Papa Francis azikwa: Siku 9 za Novendiale zaanza / Reuters
26 Aprili 2025

Papa Francis, ambaye ni Baba Mtakatifu wa 266 katika historia ya Kanisa Katoliki, ameondoka akiwa ameliongoza kanisa hilo lenye wafuasi bilioni 1.4 duniani, atakumbukwa kwa misimamo yake ya kiliberali, ambayo imewashangaza wengi, wakiwemo wa kanisa hilo duniani, hasa kutokana na kupindisha baadhi ya tamaduni ndani ya dhehebu hilo.

Papa Francis, ambaye jina lake halisi ni Jorge Mario Bergoglio, ni mzaliwa wa Argentina, akitokea shirika la Wajezuiti.
Alichagua jina la Francis, akitaga kuiga mfano wa Mtakatifu Fransisko wa Asizi ambaye aliishi maisha ya unyeyenyekevu na kujishusha.

Katika miaka yake 12 ya Upapa, Papa Francis aliteua Maaskofu 530 katika majimbo tofauti ulimweguni na Makardinali 102, ambao kati ya hao, wataingia kwenye mchakato wa kuchamgua mrithi wake mara baada ya kumalizika kwa Novendiale ambacho kinaaanza baada ya yeye kuzikwa.

Wakati wa uongozi wake ndani ya Vatican, Papa Francis atakumbukwa kwa kuzitembelea nchi 10 barani Afrika, kati ya 68 ulimwenguni, japo hakuwahi kuitembelea nchi yake ya Argentina tangu achaguliwe Machi 2013.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us